TANGAZO


Monday, November 25, 2013

Jeshi lakabiliana na wapiganaji Libya

 



Watu watatu wameuawa kwenye makabiliano kati ya wanajeshi na wapiganaji wa kiisilamu mjini Benghazi.

 
Milio ya risasi ilisikika asubuhi na mapema huku moshi mkubwa ukishuhudiwa kufuka katika baadhi ya sehemu za mji huo.

Watu kadhaa wamejeruhiwa upande wa wanajeshi pamoja na upande wa wapiganaji wa Ansar al-Sharia, kikundi cha wapiganaji kinachoshukiwa kumuua balozi wa Marekani mjini humo Christopher Stevens mwaka 2012.

Serikali imekuwa na wakati mgumu kuyadhibiti makundi ya wapiganaji yanayodhibiti sehemu za Libya.

Siku kumi zilizopita, Waziri mkuu Ali Zeidan, alitoa wito kwa makundi ya wapiganaji kuondoka mjini Tripoli, baada ya makabiliano makali kati ya wapiganaji hao na waandamanaji.

Wapiganaji hao walihusika na vurugu za kisiasa zilizozuka na kusababisha kuondolewa mamlakani kwa hayati, Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011, lakini wametakiwa na serikali kuasi upiganaji au kujiunga na jeshi ifikapo mwishoni mwaka huu.

Msemaji wa jeshi ameelezea kuwa, makabiliano yalizuka wakati kikosi maalum cha polisi wa doria waliokuwa karibu na makao makuu ya Ansar al-Sharia kushambuliwa.
Wanajeshi watatu waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa ikiwemo raia kadhaa.

No comments:

Post a Comment