TANGAZO


Wednesday, November 13, 2013

Israel kusitisha ujenzi Palestina?

 


Ujenzi wa makazi ya walowezi wa Israel Palestina
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemuagiza waziri wa Nyumba nchini humo kuangalia upya mpango wa ujenzi wa zaidi ya nyumba 20,000 katika eneo la Ukingo wa magharibi mwa mto Jordan.
Netanyahu amesema mpango huo uliotangazwa jumanne wiki hii na waziri wa Nyumba Uri Ariel unaweza kuleta mvutano usio wa lazima na jumuiya ya kimataifa kufuatia Palestina kudai kuwa watakata rufaa umoja wa mataifa Israeli.
 
Amesema mpango huo hauna mchango wowote kwa Wayahudi na unakuja wakati ambao kunafanyaika jitihada za kipindi ambacho kuna jitihada za kimataifa katika kufikia muafaka mzuri na Iran kutokana na mzozo wa muda mrefu baina yao.Netanyau pia akizungumzia jambo hilo amerejea mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia muafaka yaliyofanyika Geneva kuhusiana na kuhusiana na mpango wa Tehran.

Hata hivyo Waziri wa Nyumba wa Israel Ariel amekubaliana na ombi la Waziri wake mkuu kuhusiana na utata wa mpango huo na uwezekano wa kuweza kuahirisha mpango huo.

Palestina inataka kusitishwa kwa ujenzi huo ambapo hivi karibuni Rais wa palestina Mahmoud Abbas alitahadhalisha juu ya mpango na kudai kuwa unaweza kuathiri muafaka wa mazungumzo yanayoendelea

Palestina inataka taifa lake kujumuisha eneo lake lote pamoja na lile lililochukuliwa na Israel mwaka 1967 ambapo kwa sasa zaidiya Wayahudi 500,000 wanaishi katika makazi zaidi ya 200 katika eneo hilo la ukingo wa magharibi wa mto Jordan mashariki mwa Jerusalem

Hata hivyo pamoja na kumtaka waziri wake wa Nyumba kufikiria upya juu ya ujenzi wa makazi hayo Netanyahu amekataa kurejeshwa Palestina maeneo yanayodaiwa kuwa yalichukuliwa kabla ya mwaka 1967 na kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya mipaka.

No comments:

Post a Comment