Marekani inataraji kutangaza rasmi kulitambua kundi la
wapiganaji wa kiislamu la Boko kama kundi la kimataifa la ugaidi . Uamuzi huo
umechukuliwa leo ambapo idara za usalama za marekani zimeelekezwa kukata
mitandao ya kibiashara ya kundi hilo pamoja na njia zote za usafirishaji fedha
ili kudhibiti kupanuka kimataif.
Marekani haijalitambulisha rasmi kundi hilo kama la kigaidi japo kuwa taarifa za mashirika ya habari yanaarifiwa kuwepo kwa mpango huo wa marekani dhidi ya kundi la Boko Haram.
Kundi hili la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 huku mashambulizi yake yakielekezwa katika vituo vya jeshi,katika shule na kuendesha mapigano na vikosi vya ulinzi nchini Nigeria.
Mchambuzi wa BBC nchini Nigeria Naziru Mikailu amesema uamuzi huo wa Marekani dhidi ya Boko Haram huenda ukapokelewa kwa furaha na na serikali ya Nigeria na taasisi za kikristo ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilengwa na mashambulizi ya kundi hilo
No comments:
Post a Comment