TANGAZO


Friday, November 22, 2013

Iran: Marekani yatishia vikwazo vipya

 


Kiongozi wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei

Afisa mmoja mwandamizi wa chama cha Democrat nchini Marekani, senata Harry Reid, amesema kuwa baraza la senate litaiwekea Iran vikwazo vipya mwezi ujao, iwapo mazungumzo yanayoendelea mjini Geneva, kuhusu mpango wake wa nuklia hayatafualu.
 
Wajumbe kutoka mataifa sita yenye ushawishi mkubwa duniani, ikiwemo Marekani, zinajaribu kuafikia mkataba wa awali ambao utawala wa Tehran utasaini kuidhinisha kupunguza urutubishaji wa madini ya uranium ili jamii ya kimataifa ilegeze baadhi ya vikwazo vilivyoiwekea.
Lakini baadhi ya masineta wanasema wana wasi wasi kuwa mkataba huo hautotosha kudhibiti mpango huo wa Iran.
Baada ya siku mbili za mazungumzo mjini Geneva, mjumbe mmoja wa Iran alisema kuwa maswala muhimu yangali kujadiliwa wakati mjumbe mwingine akisema kuna umuhimu wa kuondoa kile anachosema ni vizingiti vinavyotatiza mazungumzo hayo.

No comments:

Post a Comment