Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki; George Lauwo (kushoto), Akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato jambo kwa waandishi wa habari kuhusu, kuelekea matumizi ya mfumo mmoja wa fedha, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Steven Mbundi.
Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Steven Mbundi. Akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu uliokuwa msimamo wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki uliopelekea Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa vikao vya bunge hilo, katika mzunguko wa kawaida wa nchi wanachama. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
UFAFANUZI
HIVI karibuni wananchi wengi wamekuwa wakifuatilia na kuulizia kuhusu taarifa mbali mbali zinazotolewa na vyombo vya habari juu ya hatua ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za Kenya, Uganda na Rwanda kufanya mikutano ya utatu kujadili masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pasipo kuzishirikisha nchi za Tanzania na Burundi. Mikutano hiyo inaandaliwa kupitia utaratibu wa Ushirikiano wa nchi hizo tatu kupitia Wizara za Mambo ya Nje ya Nchi zao na sio kupitia mfumo wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kulingana na taarifa
zilizotolewa kwa vyombo ya habari mara baada ya kukamilika kwa mkutano wa wakuu
wa nchi hizo tatu uliofanyika tarehe 24-25 Juni, 2013 huko Entebbe Uganda.
Masuala yaliyojadiliwa na kutolewa maamuzi na
mwongozo wa utekelezaji ni pamoja na:
1)
Ujenzi
wa Reli ya Kisasa kutoka Mombasa-Kampala– Kigali Km 2,784;
2)
Ujenzi
wa Bomba la Mafuta South Sudan-Kampala-Kenya;
3)
Ujenzi
mitambo ya kusafisha mafuta Uganda;
4)
Kuongeza
upatikanaji wa Umeme;
5)
Kuanzisha Himaya Moja ya Forodha; (single customs
Territory)
6)
Kuharakisha
Shirikisho la Kisiasa;
7)
Vitambulisho
vya Kitaifa kutumika kama Hati ya Kusafiria; na
8)
Visa ya
Pamoja ya Utalii.
UFAFANUZI
Pamoja na kuwa Ibara ya 7(1) (e) ya
Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), inaruhusu nchi
wanachama kuwa na Ubia (Bi-lateral or Tri-lateral agreements), ni lazima suala
linaloenda kutekelezwa chini ya mfumo huo liwe limejadiliwa na kukubalika na
nchi zote wanachama.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Mkutano wa 27 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika
Arusha tarehe 31 Agosti, 2013, ilitaka kujua hatma ya mtangamano wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Tanzania ilitaka ufafanuzi kutokana na ukweli kwamba baadhi
ya mambo ambayo nchi hizo zinayajadili na kuyatolea maamuzi, bado majadiliano
yake yanaendelea katika ngazi ya Jumuiya. Baraza la Mawaziri la Afrika
Mashariki lilimtaka Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri kutoa taarifa ya kina
kuhusu mikutano hii na athari zake katika Mkutano wa 28 wa Baraza la Mawaziri
unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2013.
a) KUHARAKISHA UUNDWAJI WA SHIRIKISHO LA KISIASA
Katika moja ya mikutano hiyo, Wakuu wa Nchi za
Kenya, Uganda na Rwanda walikubaliana kuharakisha uundwaji wa Shirikisho la
Kisiasa baina ya nchi hizo tatu.
Ibara ya 5(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha hatua za mtangamano wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kuwa ni Umoja wa Forodha, ukifuatiwa na Soko la Pamoja, kisha
Umoja wa Fedha, na hatimaye Shirikisho la
Kisiasa.
Kuanzia mwaka 2004 kumekuwa
na jitihada mbali mbali za kutaka kuharakisha uundwaji wa Shirikisho la Kisiasa
la Afrika Mashariki. Hii pamoja na hatua nyingine mbali mbali ilipelekea
kuundwa kwa Timu za Kukusanya Maoni ya Wananchi juu ya pendekezo hilo. Kwa
upande wa Tanzania iliundwa timu iliyokuwa na chini ya Uenyekiti wa Professa
Samweli Wangwe na matokeo yaliyoonyesha kuwa asilimia 79.4 ya watanzania
hawataki kuharakisha uundwaji wa shirikisho. Serikali ya Tanzania daima
inazingatia maoni haya ya wananchi.
Ili kuwawezesha wananchi
kujua aina ya shirikisho linalotarajiwa kuundwa, Wakuu wa nchi wanachama wa
Jumuiya waliiagiza Serikali ya Jumuiya kuunda Rasimu ya Modeli ya Shirikisho.
Na kwa sasa nchi wanachama wanafanya mashauriano ya ndani kuhusiana na rasimu
iliyowasilishwa.
VITAMBULISHO VYA KITAIFA KUTUMIKA KAMA HATI YA KUSAFIRIA
Itifaki ya Soko la Pamoja Ibara ya 9(2) Nchi
Wanachama zilikubaliana kutumia hati halali za kusafiria (Passport) katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hati hizo
ni Passport ya Nchi Mwanachama na Passport ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, imekubalika pia kuwa Nchi Wanachama ambazo zipo tayari kutumia
vitambulisho vya uraia kama hati za kusafiria zinaweza kuendelea kwa kufanya
makubaliano baina yao ili mradi tu vitambulisho hivyo viwe machine readable.
KUANZISHA HIMAYA MOJA YA FORODHA
Mwaka 2012 Wakuu wa Nchi Wanachama waliridhia
uanzishwaji wa Himaya Moja ya Forodha inayotaka bidhaa zinazopitia nchi moja
kuelekea nchi nyingine mwanachama kukaguliwa na kodi kukusanywa katika kituo
cha forodha cha kwanza bidhaa inapoingia katika Jumuiya. Masuala muhimu
yanayojadiliwa ni pamoja na kuondoa dhamana (bond) kwa mizigo iliyolipiwa kodi,
na matumizi ya njia ya kisasa ya ufuatiliaji wa misafara ya mizigo (electronic
cargo tracking system) kama njia mbadala ya matumizi ya dhamana (bond); matumizi
ya dhamana moja (single bond) kwa mizigo yote inayosafirishwa kwenda nje ya
Jumuiya na mizigo ambayo haijalipiwa kodi.
HITIMISHO
Tanzania ni sehemu ya mtangamano na nia yetu ni
kuhakikisha tunatekeleza makubaliano yetu ya pamoja kulingana na matakwa ya
Mkataba wa Uundwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Imetolewa na:
WIZARA
YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKISimu No 0222135901 au 0713341354
No comments:
Post a Comment