Ofisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), David Ndibalema (kushoto), akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mfumo wa Udhibiti wa Ubora wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kabla ya kusafirishwa (PVoC), utakaosaidia kuondoa tatizo la bidhaa hafifu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa shirika hilo, Roida Andusamile.
SHERIA
MPYA
Imebainisha hatua kadhaa iwapo inabainika kuwepo kwa bidhaa hafifu:-
Imebainisha hatua kadhaa iwapo inabainika kuwepo kwa bidhaa hafifu:-
• Kuondoa bidhaa hafifu zilizopo
sokoni;
• Kufuta leseni;
• Kuweka utaratibu wa marejesho;
• Kuharibu bidhaa duni au kuzirudisha
zilikoagizwa;
• Kutoza faini.
MAJUKUMU NA MADHUMUNIMajukumu makuu ya Shirika ni
• Kukuza matumizi ya viwango;
• Kuinua ubora wa bidhaa na huduma nchini
ili kulinda afya na usalama wa walaji, kulinda mazingira, kupanua soko la nje
kwa bidhaa zetu na kukuza uchumi;
• Kudhibiti uingiaji wa bidhaa ndani
ya nchi ili kuhakikisha ni bidhaa bora tu ndizo zinaruhusiwa kuingia nchini.
UDHIBITI WA UBORA WA BIDHAA ZINAZOTOKA NJE YA
NCHI KABLA YA KUSAFIRISHWA (PVoC)
Kuna mifumo ifuatayo katika ukaguzi wa bidhaa:
Destination Inspection (DI).
• Ukaguzi wa bidhaa unaofanyika baada
ya sherena kufika nchini kabla ya kuingia sokoni.
• Ukaguzi wa bidhaa sokoni.
• Uanzishwaji wa ofisi za TBS
mipakani.
• Ukaguzi wa mara kwa mara katika
masoko (market surveillance).
• Udhibitishaji wa makampuni ya nje
kupitia utoaji wa leseni za ubora.
• Kutambua udhibiti wa mashirika ya
Viwango ya nje.
Pre-shipment
Verification of Conformity to Standards(PVoC)
• Ukaguzi wa ubora wa bidhaa
unaofanyika kabla ya shehena kusafirishwa.
• Mfumo wa udhibiti unaotumika
kuhakiki bidhaa zinazoingizwa zinakidhi matakwa ya Viwango vya Taifa na vya
Kimataifa.
MADHUMUNI NA
FAIDA ZA PVoC
• Kuhakiki bidhaa zinazoingizwa nchini
zinakidhi matakwa ya viwango vya Tanzania au Kimataifa kabla hazijasafirishwa.
• Kulinda afya na usalama wa watumiaji
pamoja na kuzuia uchafuzi wa mazingira.
• Kuongeza ufanisi wa kuondoa shehena
bandarini na kupunguza mlundikano wa shehena bandarini (trade facilitation)
• Kulinda viwanda vya ndani dhidi ya
ushindani usio wa haki (unfair competition) unaosababishwa na uwepo wa bidhaa
zenye ubora hafifu zilizoagizwa toka nje ya nchi.
• Kwenda sanjari na mageuzi ya
teknolojia yanayofanywa na TRA na TPA, yanayolenga kuondoa mlundikano wa
shehena.
• Kuzuia Tanzania isigeuzwe jalala la
bidhaa zenye ubora hafifu.
UTEKELEZAJI WA PVoC
• Mnunuzi
wa Tanzania anatakiwa kuwasiliana na
muuzaji wake nje ya nchi, kwa kumueleza bidhaa anayoihitaji na viwango
vyake
• Muuzaji
anatakiwa kuwasiliana na wakala wa huduma za PVoC aliyepo karibu naye ili
kupata utaratibu wa kufuata kabla ya kusafirisha shehena.
• Wakala
wa PVoC hupima bidhaa husika na kutoa cheti cha ubora (CoC) endapo bidhaa hiyo
itakidhi matakwa ya kiwango.
• Wakala
wa PVoC hutuma CoC halisi (Original) kwa mnunuzi aliyeko Tanzania na nakala ya
CoC hutumwa kwa muuzaji.
• Mnunuzi
huwasilisha CoC halisi TBS kwa kuhakiki na TBS hutuma CoC hiyo TRA kwa njia ya
kielektroniki ili kuruhusu shehena kutolewa bandarini.
• TBS
inafanya ukaguzi kwa wakala wa PVoC mara moja kwa mwaka kuhakikisha kazi
imefanyika kulingana na mkataba.
UZOEFU WA NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA
• Shirika
la Viwango Kenya (KEBS) lilianza PVoC June 2005 hadi leo linaendelea kutekeleza
• Asilimia
75 ya bidhaa zinazoingia Kenya zinakidhi matakwa vya Viwango
• Kwa
Afrika, PVoC inatekelezwa Nigeria, Botswana Ethiopia, Ghana, Burkina Faso na
Uganda
HITIMISHO
• Mfumo
wa PVoC umefanikisha lengo la kuzuia bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini kwa
asilimia 65, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TBS mwezi Desemba, 2012, baada
ya kuwahoji wasambazaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi katika mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Mara na Kagera.
No comments:
Post a Comment