Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya wamewaonya waandisi wa
habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la Westgate ambako magaidi
walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi kufanya uporaji katika jengo
hilo wakati wakipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka nyara watu
waliokuweme ndani ya jumba hilo.Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema kuwa waandishi hawapaswi kutoa kuchochea Propaganda, au kuwachochea wakenya wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa habari zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya plastiki zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa na Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa operesheni yao kutoka na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri kuoka kwa wakuu wa usalama.
No comments:
Post a Comment