TANGAZO


Saturday, October 12, 2013

Waziri wa Habari, Fenella Mukangala, atembelea maonesho ya Wiki ya Vijana, Shule ya Msingi Mlandege, Iringa , Maonesho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (mwenye mavazi meusi), akiwasili katika Viwanja vya maonesho ya Wiki ya Vijana, Shule ya Msingi Mlandege, Iringa akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Wizara hiyo, Katibu Mkuu, Sihaba Nkinga (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu, Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto),Mkurugenzi wa Utamaduni Prof. Herman Mwansoko (kulia) na Mkurugenzi wa Vijana James Kajugusi (wa pili kulia).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa leo mara baada ya kuangalia maandalizi ya sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akitembelea banda la Maonyesho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo mjini Iringa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (koti jeusi) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga wakitembelea banda la maonyesho la wajasiriamali kutoka wilayani Bagamoyo wanaoshiriki maonesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.Sihaba Nkinga(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zikiwemo sabuni za kuogea ya MKIPI enye Makao yake Pemba na Zanzibar Bw. Mohamed Foum wakati alipotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo leo. (Picha zote na Aron Msigwa- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment