TANGAZO


Saturday, October 12, 2013

Naibu Katibu Mkuu Habari, atembelea Maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Vijana mjini Iringa


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia), akizungumza na Vijana pamoja na wakazi wa Manispaa ya Iringa, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwlimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.Wengine ni Mbunge wa Iringa (kupitia viti maalum), Rita Kabati (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Zanzibar, Mohamed Salim Alli.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabrie, atembelea banda la maonesho la WAMATA, kuona shughuli zinazotolewa kwa vijana hususan Ushauri nasaha na Upimaji wa Hiari wa Virus vya Ukimwi mjini Iringa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabrie na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Zanzinbar, Mohamed Salim Alli (wa tatu kulia), wakiwa na waongoza midahalo (MC) na shughuli nzima ya Maonesho ya Wiki ya Vijana katika Uwanja wa Mlandege Iringa.
Mbunge wa Iringa  Viti Maalum (CCM) Mh. Rita Kabati akiwaasa vijana kuhusu kujinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi katika Uwanja wa Maonyesho wa Mlandege wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Vijana wa Halaiki wakiendelea na maandalizi ya sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Maandalizi ya sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, yakiendelea katika uwanja wa Samora mkoani Iringa leo. (Picha zote na Aron Msigwa- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment