TANGAZO


Friday, October 4, 2013

Wapiga mbizi watafuta miili Lampedusa



Baadhi ya waliopoteza maisha yao wakitafuta kuingia Ulaya
Juhudu za uokozi zinaendelea Kusini mwa Utaliana baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Italia, kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Wapiga mbizi wamekuwa wakitafuta miili chini ya bahari katika mabaki ya boti hiyo iliyozama Alhamisi na kuleta hofu ya wahamiaji 300 kufa maji.
Hadi sasa miili 111 imepatikana na watu wengine 200 waliokuwa miongoni mwa wahmiaji 500 waliokuwa wanakwenda Ulaya bado hawajapatikana.
Boti hiyo ilizama ikiwa imesalia na kilomita moja kufika katika ufuo wa bahari siku ya Alhamisi.
Kwa mujibu wa maafisa wa uokozi, idadi kubwa ya miili ya wahamiaji hao inaaminika kuwa ndani ya boti hiyo iliyozama.
Zaidi ya watu 150 waliokolewa. Wengi wa waliokuwa katika boti hiyo walikuwa raia wa Somalia na Eritrea wakiwa katika safari ya kutafuta hifadhi nchini Utaliana. Inaaminika boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 500
Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya Utaliana ,mmiliki wa boti hiyo ambaye ni raia wa Tunisia alikamatwa
Aliwahi kufukuzwa kutoka nchini humu mnamo mwezi Aprili.
"Huu sio mkasa wa Italia, ni mkasa wa Ulaya na sharti kisiwa cha Lampedusa kionekana kuwa kitovu cha kuingilia Ulaya wala sio Utaliana tu,'' alinukuliwa akisema afisaa mmoja wa serikali .
Kote nchini Utaliana, kutakuwa na kimya cha dakika moja kuwakumbuka walioangamia.
kwa sababu ya kutokuwa na stakabadhi zinazohitajika, njia pekee ya wahamiaji wa kiafrika kufika Ulaya ni kupitia baharini kwa kusaidiwa na makundi ya wahalifu.
Mwandishi wa BBC Allan Johnston anasema kuwa wakati huu ambapo,mawimbi ya bahari ya Mediterranea yanakuwa yametulia, mamia ya wahamiaji huwasili katika fuo za kisiwa hicho karibu kila siku.

No comments:

Post a Comment