TANGAZO


Friday, October 4, 2013

Misri kusimamia mali ya Brotherhood


Wafuasi wengi wa Muslim Brotherhood wamekamatwa na kuuawa lakini baadhi wangali wanajitokeza kuandamana
Serikali ya Misri imechukua hatua ya kupiga tanji na kuchukua mali ya vuguvugu la Muslim Brotherhood baada ya harakati za kundi hilo kuharamishwa kufuatia msako mkubwa uliofanywa na serikali.
Imesema kuwa itaharamisha au kuchukua usimamizi wa huduma ambazo zilikuwa zinatolewa na vuguvugu hilo ikiwemo za hospitali, shule na huduma nyingine za kijamii.
Hatua ya serikali ya kuharamisha shughuli za kundi hilo ilikuja baada ya mahakama kuamua hivyo lakini imethibitishwa kutokana na rufaa za chama hicho.
"Kulingana na sheria, msitari wa mwisho unasema sasa wameharamishwa,” alisma afisaa mmoja wa serikali.
Kwa mujibu wa msemaji wa waziri wa maswala ya kijamii, ambaye ndiye alichukua hatua ya kuharamisha vuguvugu hilo, baraza la mawaziri liliafikiana kuunda kamati kuchunguza chanzo cha ufadhili wa vuguvugu hilo na kutaifisha mali zake.
Alisema kuwa ikiwa mipango ya chama hicho itagundulika kuwa na uhusiaono wowote na vuguvugu la Muslim Brotherhood – iwe ya elimu au kiafya , basi uamuzi utafanywa na mahakama na serikali kuzisimamia.

'Kuwajibishwa’

Kipindi cha siku 15 cha kukata rufaa dhidi ya hatua ya mahakama kinakwisha Jumatatu , lakini hatua zilichukulilwa mapema ili mawaziri wajizuie kukutana kwa siku tatu zijazo ambazo ni siku za mapumziko.
Muslim Brotherhood waliingia mamlakani miezi 14 iliyopita lakini jeshi likamwondoa mamlakani aliyekuwa rais, Mohammed Morsi, na hajaonekana hadharani, tangu mwezi Julai kufuatia maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.
Wengi wa viongozi wa vuguvugu hilo wako jela na linasema kuwa wafuasi wake wengi wameuawa katika misako ya polisi na jeshi.
Licha ya hatua ya serikali kuharamisha chama, wafuasi wa Brotherhood wanaendelea kujitokeza barabarani kuandamana ingawa idadi yao ni ndogo sana ikilinganishwa na siku za nyuma.
Chama ambacho kimekuwa kikikandamizwa kwa miaka mingi , sasa kwa mara nyingine kinalazimishwa kujiondoa kutoka ulingo wa siasa , lakini bila shaka kitasalia kuwepo.

No comments:

Post a Comment