Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GODTEC(T) Limited Bwana Abnery Shagille akielezea jambo kwa washiriki wa semina ya wadau wa maendeleo kutoka Manispaa ya Kinondoni kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi semina hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sparke International Bwana Gerald Magooge Reuben akielezea namna alivyofanikiwa kuanzisha kampuni yake kwa msaada mkubwa wa GODTEC ambapo kupitia mpango wake wa Kiota cha Utajirishaji uwasaidia vijana kuanzisha miradi ya uzarishaji mali.
Mkurugenzi wa Ubunifu,Uendelezaji na Ufuatiliaji wa GODTEC Bwana Aloyce Maganga akitoa mada kuhusu namna mfumo wa utajirishaji uanvyo weza kutekelezwa na wadau wa maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu namna ya utekelezaji wa mfumo wa utajirishaji wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inafundishwa na mmoja wa watoa mada katika (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu namna ya utekelezaji wa mfumo wa utajirishaji wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inafundishwa na mmoja wa watoa mada katika (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na Uhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven Kissui na viongozi wa GODTEC wakiwa katika picha ya pamoja na Vijana walioanzisha Kampuni ya Sparke International waliokaa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na Uhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven Kissui akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kuhusu mfumo wa utajirishaji iliyoandaliwa na Kampuni ya GODTEC (T) Limited. (Picha zote na: Frank Shija - WHVUM)
Na Frank Shija - WHVUM
Vijana wametakiwa kuwa wabunifu na wenye fikra za kimkakati katika kutumia fursa zilizopo na kujiajiri kwa kutumia taaluma na ujuzi mbalimbali walionao badala ya kuendelea kusubili ajira za Serikali.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana kitengo cha Uwezeshaji na Uhamasishaji wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven Kissui alipokuwa
akifungua semina ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa Kata kuhusu mfumo wa utajirishaji.
Dkt. Kissui amesema kuwa huu si wakati wa kijana kukaa kijiweni na kuwataka wabadilike na kuachana na
mawazo hasi yanayopelekea kukaa vijiweni wakisubili ajira za Serikali pekee na kuacha fursa nyingi bila
kutumika.
“Inashangaza sana kumuona mtu ana ujuzi na taaluma nzuru lakini anakaa kijiweni anasubiri Serikali itangaze
kazi, vijana badilikeni!tumieni fursa zilizopo hapa nchini nanyi mtakuwa mmejikomboa katika janga la umaskini”, alisema Dkt. Kissui.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GODTEC (T) Limited Bwana Abnery Shagille amesema kuwa vijana wanapaswa kutambua kuwa Serikali imetimiza wajibu wake wa kutengeneza ajira kwa vijana kwa kuwa imeweka sera na sheria madhubuti ambazo zinatoa fursa kwa mwananchi kujiajiri.
Aidha Shagille ameongeza kuwa Kampuni yake imeamua kuchukua jukumu la kutafsiri sera zilizopo ili
jamii ione fursa zilizopo na hatimaye wachukue hatua ya kutumia fursa hizo badala ya kuendelea kulalamikia
Serikali.
Ameongeza kuwa mpaka sasa kampuni yake imeweza kuwasaidia vijana waliohitimu vyuo mbalimbali kujiajiri kwa kuanzisha makampuni yao wenyewe baada ya kupewa mafunzo maalum ambayo utolewa na GODTEC.
Alizitaja kampuni hizo za vijana kuwa ni Sparke International na Brecco zote za jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Sparke Internation Bwana Gerald Magooge Reuben ameisema kuwa kupitia GODTEC wamefanikiwa kuanzisha kampuni hii na kuondokana na tatizo la ajira baadala yake nao wemekuwa waajiri.
Semina kwa maafisa maendeleo ya jamii, maafisa watendaji wa kata na wakuu wa vitengo kutoka manispaa ya Kinondoni imeandaliwa na Kampuni ya GODTEC kwa lengo la kushirikisha watendaji kati mfumo wa uwekezaji unaojulikana kwa jina la Tajirisha ambao unamuwezesha kijana kumiliki biashara yake.
No comments:
Post a Comment