Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anasema kuwa atashirikiana na
mwenzake wa Sudan Kusini kutatua mgogoro kuhusu eneo wanalozozania la Abyei.
Bwana al-Bashir alisema kuwa anataka mwafaka utakaokubalika kwa watu wa Abyei
kupatikana.Hali ya Abyei haijajulikana tangu Sudan Kusini kujipatia uhuru mwaka 2011.
Watu wa kabila la Ngok Dinka -- walio na uhusiano na Sudan Kusini wanajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu ikiwa watakuwa upande wa Sudan au Sudan Kusini.
Watu wa kabila la kiarabu wa Misseriya -- ambao pia wanaishi katika eneo hilo -- hawatashiriki kwenye kura hiyo ya maoni.
Muungano wa Afrika mnamo siku ya Jumapili waliituhumu serikali ya Sudan kwa kuzuia wajumbe wa muungano huo kuzuru eneo la Abyei.
Wanasema kuwa hawatakubali matokeo ya kura hiyo ya maoni.
Hatua hii ikiwa itafanyika, bila shaka itasababisha taharuki zaidi katika jimbo la Abyei , moja ya chanzo cha mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Hakuna mmoja kati ya nchi hizo anataka kukosa udhibiti wa jimbo hilo, hasa kwa sababu ya visima vya mafuta vilivyoko katika jimbo lenyewe ingawa visima vyenyewe vinadidimia.
Pia kuna ardhi yenye dhoruba.
Bashir kweli amesema kuwa atashirikiana na mwenzake Salva Kiir. Lakini je anaweza kukubali kupoteza Abyei, hususan anapokabiliwa na maandamano dhidi ya utawala wake ?
No comments:
Post a Comment