Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua zinazochukuliwa na Shirika hilo, katika kutatua tatizo la makazi nchini, ikiwa ni pamoja na mkakati wa miaka 5, utakaohusisha ujenzi wa nyumba 15,000 za bei nafuuu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Frank Mvungi. (Pcha zote na Hassan Silayo-MAELEZO na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Willium Genya akitoa wito kwa wananchi kupitia kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kujitokeza kununua nyumba hizo, ili shirika hilo, liweze kutimiza azma pamoja na sera ya kuwapatia wananchi makazi na kuondoa kabisa tatizo la makazi nchini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika hilo, Muungano Saguya.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua zinazochukuliwa na Shirika hilo, katika kutatua tatizo la makazi nchini, ikiwa ni pamoja na mkakati wa miaka 5, utakaohusisha ujenzi wa nyumba 15,000 za bei nafuuu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Willium Genya.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua zinazochukuliwa na Shirika hilo, katika kutatua tatizo la makazi nchini, ikiwa ni pamoja na mkakati wa miaka 5, utakaohusisha ujenzi wa nyumba 15,000 za bei nafuuu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Willium Genya.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua zinazochukuliwa na Shirika hilo, katika kutatua tatizo la makazi nchini, ikiwa ni pamoja na mkakati wa miaka 5, utakaohusisha ujenzi wa nyumba 15,000 za bei nafuuu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Willium Genya na kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Frank Mvungi.
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Willium Genya akitoa wito kwa wananchi kupitia kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kujitokeza kununua nyumba hizo, ili shirika hilo, liweze kutimiza azma pamoja na sera ya kuwapatia wananchi makazi na kuondoa kabisa tatizo la makazi nchini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika hilo, Muungano Saguya na kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Frank Mvungi.
1.0 UTANGULIZI:
•
Awali ya yote, ningependa kuwapa kwa muhtasari
hali ya ujenzi wa nyumba ilivyokuwa tangu kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba la
Taifa, kabla sijaelezea jinsi tuliweza kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka
2010 ya Chama Tawala.
•
Tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Rais wa
kwanza wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alithamini vitu vitatu
vinavyoleta utu na maendeleo ya binadamu. Vitu hivyo ni chakula, mavazi na
malazi. Kutokana na imani ya Mwalimu kuwa makazi ni sehemu ya utu wa binadamu,
alilianzisha Shirika la Nyumba la Taifa mwaka 1962 ili kuwajengea wananchi
hususan wa kipato cha chini nyumba bora.
•
Hadi
kufikia mwaka 1975, likitumia ruzuku ya Serikali, mikopo kutoka Benki ya Nyumba
(THB) iliyoanzishwa mwaka 1973 na misaada kutoka Serikali ya Shirikisho ya
Jamhuri ya Ujerumani Magharibi (FRG), Shirika hili lilifanikiwa kujenga
nyumba 14,462 nchini kote nyingi
zikiwa zimejengwa wakati wa oporesheni ondoa makuti (slum clearance). Asilimia
90 ya nyumba hizi zilikuwa ni nyumba za gharama nafuu.
•
Kufikia mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni
mwa miaka ya 80, Shirika hili lilishindwa kutekeleza kazi zake za ujenzi
kutokana na hali ngumu iliyoikumba nchi yetu na dunia kwa ujumla. Hali
hiyo ilsasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia na vita
vya Kagera. Uwezo wa Serikali ukawa mdogo na hali ya makazi ikazidi kuwa
mbaya huku idadi ya watu wanaokimbilia mijini kutafuta maisha bora nayo
ikiongeza ukubwa wa tatizo la nyumba. Nayo kodi ya nyumba za NHC iliyokuwa
ikichangia asilimia 80 ya mapato yake, ambayo ilikuwa ndogo kutokana na ruzuku
iliyokuwa ikitolewa na Serikali, ikaendelea kuwa hivyohivyo kwa kuwa Sheria ya
Zuio la Kodi Na. 17 ya mwaka 1984 ilizuia kupandisha kodi. Hata pale Shirika
lilipotaka kurekebisha kodi zake ili liweze kujiendesha na kutengeneza nyumba
zake, ilipata upinzani mkubwa kutoka kwa wapangaji wake waliosaidiwa sana na
Sheria hiyo. Hali hii ililifanya Shirika kujenga tu nyumba 1,664 kutoka kipindi
cha mwaka 1976 hadi 1990.
•
Katika kuhakikisha kuwa sekta ya nyumba inaleta
tija ya kiuchumi na kijamii hapa nchini, mwaka 1990 Serikali ililiunganisha
Shirika hili na iliyokuwa Msajili wa Majumba ya Mwaka 1971. Pamoja na
kuunganishwa kwa mashirika haya mawili yaliyokuwa yakifanya kazi zinazofanana,
bado sheria mbalimbali na kukosekana kwa mikopo ya fedha za kujenga au kununua
nyumba, kuliidumaza NHC na kufanikiwa kujenga nyumba 600 tu hadi kufikia mwaka
2010.
•
Ili kuondoa kusuasua kwa sekta ya nyumba
nchini, mwaka 2005 na 2008, Serikali ilijitahidi kubadilisha sheria mbalimbali
zilizokwamisha uwekezaji katika sekta ya nyumba. Sheria hizo ni pamoja na
sheria ya ardhi ya mwaka 1999, sheria iliyolianzisha Shirika la Nyumba la
Taifa, sheria ya mikopo ya nyumba na sheria ya hati pacha katika majengo ya
ghorofa.
•
Aidha, mwaka 2010, Serikali iliazimia kuliunda
upya Shirika hili kwa kulipatia uongozi mpya, ambao umetengeneza Mpango Mkakati wa miaka mitano
2010/11-2014/15 ambao umejikita katika kuwezesha ujenzi wa nyumba 15,000 katika
kipindi hicho, idadi ambayo haijawahi kutekelezwa kwa kipindi kifupi na Shirika
hili tangu lianzishwe mwaka 1962. Lengo
ni kuhakikisha kuwa kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine zikiwemo
taasisi za fedha, NHC inashiriki kikamilifu kuondoa uhaba wa nyumba hapa nchini
ambao kwa sasa unafikia nyumba milioni 3 na ukiongezeka kwa nyumba 200,000 kwa
mwaka.
•
Katika kutekeleza hilo, Shirika limeweka
msukumo wa pekee katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za kuwauzia wananchi
wa kipato cha kati na chini. Katika kuongeza msukumo wa jambo hili, Serikali
sasa inaliunga mkono sana Shirika na mwezi Juni mwaka 2012 Mjini Dodoma,
Mheshimiwa Rais Dk. Jakaya Kikwete, aliunda Kamati ya Viongozi kutoka Taasisi
mbalimbali za Umma ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, kuangalia namna ya kuanza
utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini. NHC katika Kamati hiyo
ni Katibu na mratibu wa utekelezaji wa maagizo hayo ya Mheshimiwa Rais.
2.0 UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI:
Kutokana
na mpango mkakati wa Shirika na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya ya CCM ya
mwaka 2010, pamoja na maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Shirika limeagizwa kufanya yafuatayo:-
Ibara ya (iii) ya Ilani ya Uchaguzi inalitaka Shirika kuhakikisha kuwa jumla ya nyumba 15,000 (kwa
wastani nyumba 3,000 kila mwaka) zinajengwa na kwa kushirikiana na sekta
binafsi.
• Katika kutekeleza hilo, Shirika limekamilisha matayarisho ya miradi 65 yenye jumla ya nyumba za makazi 17,078 ambazo ni za gharama nafuu, kati na juu, zilizoanza kujengwa
kwenye maeneo mbalimbali nchini. Kiasi cha 70%
ya nyumba zinazojengwa kitauzwa na 30%
kitapangishwa. Hadi kufikia Septemba, 2013, ujenzi wa miradi saba (7) yenye jumla ya nyumba
657 ulikamilika; ujenzi wa miradi 14
yenye jumla ya nyumba 980 ulikuwa unaendelea; na ule wa miradi
30 yenye jumla ya nyumba 3,096
ulitarajiwa kuanza katika kipindi cha 2013/14.
Aidha, Shirika lilikamilisha miradi
miwili (2) ya majengo ya biashara iliyoko Dar es Salaam na Kigoma na
kuendelea na ujenzi wa miradi minne (4)
iliyoko katika mikoa ya Morogoro, Musoma na Mbeya. Ujenzi wa miradi 12 mingine ya majengo ya
biashara unatarajiwa kuanza katika mwaka 2013/14. Vile vile, Shirika kwa
kushirikiana na waendelezaji binafsi,
lilikamilisha miradi 11 ya majengo
ya biashara na makazi kwa njia ya ubia na liliendelea na ujenzi wa miradi 20.
Katika
kipindi hiki, tulikamilisha pia Miradi mitatu (3) yenye jumla ya nyumba za kuuza 84 iliyoanza katika
maeneo ya Kibla – Arusha (nyumba 48), Haile Selasie – Arusha (nyumba 4) na Mbweni
JKT – Dar es salaam (nyumba 34). Katika kipindi hiki shirika pia liliweza
kukamilisha mradi wa jengo la biashara lenye ghorofa nne (4) lililoko mtaa wa
Lumumba mjini Kigoma kwa gharama shilingi bilioni 2.53. Ujenzi wa jengo hili
ulianza mnamo Januari, 2010 na kukamilika mwezi Machi, 2012
Ibara ya (viii) ya Ilani ya Uchaguzi inalielekeza Shirika
la Nyumba la Taifa kuwa mwendelezaji ardhi mkubwa (Master Estate Developer) na kujenga nyumba
nyingi kwa ajili ya kuuza au kupangisha kwa wananchi wote na hasa watu wa
kipato cha kati na cha chini.
·
Katika
kutekeleza hilo, Shirika lilianza kwa
kununua ardhi, kuipima na kupanga maeneo. Lengo la mkakati huu ni
kuendeleza maeneo kwa kujenga nyumba na
majengo ya biashara na kuuza baadhi ya
viwanja kwa waendelezaji wengine. Hadi kufikia Septemba, 2013, Shirika lilikuwa limekamilisha ununuzi wa ekari 1,210.58 na viwanja 457. Upimaji, upangaji na utayarishaji wa michoro ya
majengo, nyumba na miundombinu kwa maeneo ya Usa River – Arusha (ekari 296), Burka – Arusha (ekari 573), Iyumbu – Dodoma (ekari 236) na Kibada/Uvumba – Dar es
Salaam (ekari 202), ulikuwa
unaendelea. Ili Shirika liweze kutekeleza jukumu la kuwa Mwendelezaji Mkuu kwa
ufanisi, limeiomba Serikali ruksa ya kuwa Mamlaka ya kupanga matumizi ya ardhi (planning
authority).
•
Shirika hivi sasa limeanza kwa kasi kutekeleza
ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri mbalimbali za Miji na
Wilaya. nchini. Ili kufanikisha
hilo, Shirika limekuwa katika hatua mbalimbali za ununuzi wa jumla ya ekari 18,421 kwenye Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini kwa
ajili ya kujenga nyumba hizi za gharama nafuu Hadi hivi sasa nyumba zipatazo 2500 ziko
katika hatua mbalimbali za ujenzi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri za
Miji na Wilaya zikiwemo Kibada-Temeke, Mvomero, Mkinga, Lindi,
Mkuzo- Ruvuma, Bombambili-Geita, Mlole-Kigoma, Ilembo-Katavi, Kongwa,
Unyankumi-Singida na Mrara-Babati. Awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba hizi
inafuata katika maeneo ya Sumbawanga, Mwongozo- DSM, Longido, Uyui, Manyara,
Kibada awamu ya pili-DSM, Monduli, Buswelu-Mwanza, Chalinze, Kyerwa, Muleba,
Iwambi-Mbeya, Mbarali na Masasi. Lengo la Shirika ni kuhakikisha kuwa kila
Halmashauri ya Wilaya na Miji hapa nchini inafikiwa na mradi huu katika mwaka
huu wa fedha.
•
Ujenzi wa nyumba hizi utawapatia makazi bora
wananchi wapatao 7285 na ajira za moja kwa moja zipatazo 7170. Aidha, kutakuwa
na huduma za kijamii zenye eneo la mraba 58,300 zikijumuisha maduka, shule,
hospitali, viwanja vya kuchezea watoto na vituo vingine mbalimbali. Gharama ya
utekelezaji wa miradi hii ni shilingi bilioni 53.8. Gharama za kuweka
miundombinu ya umeme, barabara na maji pekee ni bilioni 10.8. Hivyo, ili kuzifanya nyumba zinazojengwa kuwa
za gharama nafuu, ni muhimu taasisi zote zinazohusika na uwekaji wa miundombinu
muhimu kama umeme, barabara na maji kutimiza wajibu wao katika maeneo yote
yanayojengwa nyumba mpya. Aidha, Halmashauri za miji na Wilaya ni vema
zikasaidia kulipatia Shirika ardhi isiyokuwa na masharti yoyote ya kuwezesha
kujenga nyumba hizi. Hii ni pamoja na Mamlaka za Miji kuwawezesha kupata kwa
haraka vibali vya ujenzi ili kufanya gharama za ujenzi zisiongezeke pindi
wanapochelewa kuanza mradi husika.
• Katika
kipindi hiki, Shirika limeshiriki kikamilifu katika kusaidia juhudi za Serikali
za kuondoa umaskini nchini. Kwa kuzingatia umuhimu wa kundi la vijana katika
mustakabali wa amani na utulivu wa Taifa letu, Shirika limetengeneza sera ya
kuhudumia Jamii, iliyojikita zaidi katika kusaidia vikundi vya vijana ili
waweze kutengeneza matofali yatakayotumika kujenga nyumba za gharama nafuu.
Hivi karibuni Shirika hili liliingia makubalianao na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi
Stadi (VETA) ya kuwatumia vijana waliyohitimu VETA kutengeneza matofali katika
kanda tano zenye miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakitumia mashine
za kisasa za Hydraform. Mradi huu utasaidia kutengeneza matofali…………. yenye thamani ya shilingi bilioni
………………
•
Aidha, Shirika hili kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 1962,
limeamua kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuondoa umaskini kwa
kutoa mashine za kufyatulia tofali 640 kwa Halmashauri zote za Wilaya na Miji
160 zilizoko nchini mwetu. Mashine hizo zitatumiwa na vikundi vya vijana
vitakavyoundwa na Halmashauri hizo, kila Halmashauri ikipewa msaada wa mashine
nne (4) ambazo, kila mashine itakuwa ikihudumia vijana wapatao kumi.
Katika
mpango huo unaogharimu shilingi milioni 650, zitapatikana ajira ya moja kwa
moja kwa vijana wapatao 6,400 katika Halmashauri zote 160. Aidha, vijana hao
wataweza kuzalisha ajira zaidi ya 200,000 kutokana na kazi za ujenzi
zitakazofanywa na wananchi kwa kutumia matofali yatakayotengenezwa na vijana
hao. Kadhalika, vikundi hivyo vya vijana vitaunda SACCOS zao na hivyo kupanua
shughuli zao za kiuchumi. Pamoja na msaada wa mashine hizo, Shirika litatoa
Shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila Halmashauri kama kianzio cha vijana hao
kununua vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya kufyatua matofali kuanza.
Ili
kufanikisha mpango huo wenye maslahi makubwa kwa vijana, na nchi yetu, Shirika
kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) iliyo
chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na VETA litatoa
mafunzo ya siku 21 kuanzia mwezi Desemba 2013 hadi Januari 2014 kwa wataalam
wapatao 50, wawili kutoka kila Mkoa ambao baadae watatumika kutoa mafunzo kwa
vijana katika Halmashauri za Wilaya na Miji kuanzia mwezi Januari hadi Juni
2014. Mafunzo hayo yanahusu namna ya
kutumia mashine hayo na udongo unaofaa katika kutengenezea matofali.
3.0
MIKAKATI ILIYOWEZESHA UTEKELEZAJI WA ILANI
Katika
kuwezesha utekelezaji wa Ilani hii mikakati ifuatayo ilitumika:-
• Kuwa na mpango mkakati wa miaka mitano 2010/11 hadi
2014/15 ambao umekuwa ni dira ya kuongeza ufanisi na kutekeleza mipango
tuliyojiwekea
• Kuungwa mkono na Serikali katika kusukuma mbele ajenda
ya nyumba.
• Utafutaji wa mtaji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba- Serikali kupitia Wizara ya fedha
ililiruhusu Shirika kukopa kiasi cha shilingi bilioni 300 kutoka katika
mashirika mbalimbali ya kifedha. Kutokana
na kibali hiki, benki 15 za ndani na nje ya nchi zilikubali kukopesha Shirika
kiasi cha shilingi bilioni 310. Hadi Juni 2012, Shirika liliiingia mikataba na
benki tisa (9) zilizokubali kutoa kiasi cha shilingi bilioni 165.4 kwa ajili ya
kuongeza hazina ya ardhi na miradi ya ujenzi wa nyumba.
• Sambamba na juhudi hizo, Shirika pia liliingia
mikataba na benki (8) nchini kwa ajili ya kuwakopesha wanunuzi wa nyumba za Shirika.
Benki hizi zimeanza kutoa mikopo kwa wanunuzi wa nyumba za Shirika na kuwezesha
kasi ujenzi wa nyumba kuwa kubwa hivi sasa.
• Kuwa na mkakati wa kuzungusha fedha zinazopatikana kwa kuuza nyumba hata kabla ya ujenzi kukamilika (pre - sale) kuswezesha ujenzi wa nyumba bila kutegemea mikopo mikubwa ya taasisi za fedha.
• Kuwa na mkakati wa kuzungusha fedha zinazopatikana kwa kuuza nyumba hata kabla ya ujenzi kukamilika (pre - sale) kuswezesha ujenzi wa nyumba bila kutegemea mikopo mikubwa ya taasisi za fedha.
• Kuwa na utaratibu wa kushirisha mapato ya Shirika na taasisi
binafsi (revenue sharing model) utaratibu unaowezesha kuwekeza mtaji mkubwa
kujenga majengo makubwa ya kisasa.
• Kujenga nidhamu ya kazi na uadilifu wa wafanyakazi
wetu hali iliyofanya wadau mbalimbali kuliunga mkono Shirika. Kwa sasa
malalamiko yaliyoelekezwa kwenye Shirika na wananchi mbalimbali yamepungua
sana
• Kudhibiti mapato ya Shirika kwa kuhakikisha kodi ya
nyumba inalipwa na kila mpangaji na kwamba wote waliyonufaika na nyumba za
Shirika kinyemela wamekatiwa mirija hiyo na mapato stahiki kuingia katika
mapato ya Shirika.
• Kupungua kwa kesi zilizokuwa zikitishia uhai wa mapato
ya Shirika. Kesi hizi zilifunguliwa na watu wajanjawajanja ambao walitumia
udhaifu wa Watendaji wa Shirika kushinda kesi kirahisi hata kama hawakuwa na
uhalali wa kesi hizo. Baada ya kuona kuwa Shirika liko imara katika kusimamia
kesi zake, watu wengi waliolifungulia kesi Shirika wamefuta kesi hizo au
kuzimaliza nje ya mahakama.
4.0 MWISHO:
Ndugu
Wanahabari, kama mnavyofahamu, sekta ya nyumba ni sekta mtambuka katika
maendeleo ya uchumi. Sekta ya nyumba husaidia kuleta maendeleo ya haraka ya
sekta zinginena kutoa ajira. Taifa linalozingatia sekta ya nyumba huwezesha
nchi yao kuwa na amani, kwani mtu mwenye makazi bora, huthamini uwepo wa amani.
Hivyo, natoa wito kwa wadau mbalimbali kuithamini na kuisaidia sekta hii ili
iweze kuleta tija kwa maisha ya watanzania wengi. Natoa rai kwa taasisi zingine
kuona umuhimu wa kusaidia Shirika letu kuweza kujenga nyumba hususan za watu wa
kipato cha chini na kati ili kwa pamoja tuweze kujenga jamii huru yenye amani
na siha njema.
NEHEMIAH KYANDO MCHECHU, MKURUGENZI MKUU
No comments:
Post a Comment