Baadhi ya Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao hicho kimefanyika leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Serikalini (kushoto) na Wajumbe kutoka Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni (Kulia) wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao hicho kimefanyika leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Maalum.
SEREKALI imekutana na Kituo cha Demokrasia nchini
ambacho wanachama wake ni vyama vyenye wawakilishi Bungeni ili Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ambayo vyama hivyo viliyawasilisha Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013.
Akiongea wakati wa kikao hicho leo, Katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini
Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge ),
Mhe. William Lukuvi (Mb) alifafanua kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili na
kuchambua Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya katiba ambayo waliombwa wayawasilishe rasmi.
“Kikao hiki
kinafanyika kufuatia kikao alichofanya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete tarehe 15 Oktoba Ikulu Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Vyama
vyenye wawakilishi Bungeni na kuwaomba wawasilishe rasmi maoni yao Serikalini
na sasa kamati ya kitaalam ya Serikali tumekutana nao kujadili na kuchambua
Mapendekezo yao” alisema Lukuvi.
Vyama vya Siasa
vilivyo shiriki katika kikao hicho ni; CCM, CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi,
UDP na TLP, kwa upande wa Serikali iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Waziri
wa Sheria na Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Msaidizi wa Sheria wa
Rais, Msaidizi wa Sheria wa Waziri Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment