TANGAZO


Thursday, October 10, 2013

Rais Kikwete atembelea Kituo cha Afya Bagamoyo (IHI)


Advo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Advocatus Kakorozya akimwelezea jinsi tasisi inavyotumia teknologia kupata taarifa mbalimbali za afya ambazo zimesaidia sana serikali kutunga sera. Rais Jakaya Kikwete jana (Jumatano) alitembelea kituo cha Bagamoyo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) na kuonyeshwa kazi mbalimbali za utafiti zinazofanyika kituoni hapo. Raisi Kikwete aliisifia taasisi hiyo kwa kufanya kazi kubwa hasa katika upande wa ugonjwa wa Malaria na kujipatia sifa kubwa duniani.

Govella

Rais Kikwete akimsikiliza mtafiti wa IHI, Dk. Nico Govella akimpa maelezo juu ya utafiti wake ambapo magunia ya katani yakichanganywa na kemikali fulani yanaweza kutumika kukinga wanadamu dhidi ya mbu wanaoeneza malaria.

Grace

Rais Kikwete akimsikiliza Grace Mwangoka wa IHI akimweleza shughuli mbalimbali za maabara kwenye taasisi hiyo.

Joseph

Rais Kikwete akimsikiliza Joseph Madata ambaye ni mkutubi akimwelezea matumizi ya maktaba mtandao (digital library) ya taasisi hiyo.
Group

Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa IHI pamoja na wenzao kutoka Equatorial Guinea ambao wapo kwenye kituo hicho cha Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo.

No comments:

Post a Comment