Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akiwasili Mlimani City huku akipokelewa na uongozi wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho ya sekta ya nyumba, Ofisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula (kulia), Mkurugenzi wa Maandalizi wa maonesho hayo, Zenno Ngowi (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya kwa ajili ya kuyafungua maonesho hayo, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja Ukuzaji Biashara wa Kampuni ya Cam Gas, Suleiman Amour, akimpatia Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, maelezo kuhusu kampuni hiyo na bidhaa zake za gesi pamoja na majiko ya gesi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo, wakati alipofika kwa ajili ya kuyafungua maonesho hayo jana. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Imani Kajula.
Meneja Ukuzaji Biashara wa Kampuni ya Cam Gas, Suleiman Amour, akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu jiko la gesi la kampuni hiyo.
Meneja Mikopo ya Nyumba wa Benki ya CRDB, Silas Katemi, akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu mikopo ya nyumba inayotolewa na benki hiyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Imani Kajula.
Mtaalamu wa Ubora wa Kiwanada cha Tanga Cement, Dotto Makoye akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu mawe na dawa zingine zinazotumika katika kuzalishia cement bora ya Simba Cement kwenye kiwanda hicho, wakati alipotembelea banda la kiwanda hicho kwenye maonesho hayo jana. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Imani Kajula.
Mhandisi Ujenzi Mwandamizi wa Mfuko wa PSPF, Eng. Ally Shanjirwa, akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu mfuko huo na shughuli zake pamoja na ujenzi wa majengo yake pacha yaliopo barabara ya City Drive jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Imani Kajula.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Global Land Solutions, Murtaza Adamjee, akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu ujenzi wa nyumba za biashara zinazojengwa na kampuni hiyo.
Meneja Uelimishaji jamii na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Njela Mziray, akimpatia maelezo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), wakati alipotembelea banda hilo, mara baada ya kuyafungua maonesho ya siku mbili ya vifaa vya nyumba ya Home Expo 2013, Mlimani City, Dar es Salaam jana.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akipimwa urefu na Dk. Saleh Kinyoro wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, wakati alipotembelea banda hilo, mara baada ya kuyafungua maonesho ya siku mbili ya nyumba ya 'Tanzania Homes Expo 2013', Mlimani City, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maandalizi wa maonesho hayo, yaliyoandaliwa na Kampuni za EAGgroup, Zenno Ngowi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Imani Kajula, Sr. Mectilda Ndyamukama na Meneja Uelimishaji jamii na Masoko wa mfuko huo, Njela Mziray.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe kuyazindua maonesho ya Sekta ya Nyumba, Mlimani City, Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni uongozi wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula (wa pili), Mkurugenzi wa Maandalizi wa maonesho hayo, Zenno Ngowi (wa tatu kushoto) pamoja na baadhi ya wawakilishi wa kampuni mbalimbali zilizoshiriki katika maonesho hayo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuyafungua maonesho hayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, Imani Kajula, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuzinduliwa maonesho hayo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, jijini jana.
Uongozi wa juu wa Kampuni za EAGgroup, waandaaji wa maonesho hayo, ukiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kufunguliwa maonesho hayo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hizo, Imani Kajula na kulia ni Mkurugenzi wa Maandalizi wa maonesho hayo, Zenno Ngowi.
Maofisa wa Benki ya CRDB, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment