Jeneza lenye mwili wa Anthery Mushi likiwa katika sehemu ya kuagia, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati wa kuagwa mwili huo, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwili wa Anthery Mushi ukiwa katika sehemu ya kuagia, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati wa kuagwa mwili huo, Dar es Salaam leo.
Waombolezaji wakisikiliza maelezo ya marehemu Anthery Mushi kabla ya kuagwa.
JUU NA CHINI, Waombolezaji wakipita mbele ya jenenza lenye mwili wa aliyekuwa mwandishi na mchumba wa mwandishi wa luninga ya ITV, Ufoo Saro, Anthery Mushi, aliyejipiga risasi mbili baada ya kumuua mama wa mchumba wake huyo na pia kumpiga risasi mchumba wake, wakati wa kuaga mwili wake, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam LEO, kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi mazishi, yatakayofanyika kesho.
Waombolezaji wakilibeba jeneza lenye mwili wa Anthery Mushi, mara baada ya kuagwa, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam leo.
Gari lililoubeba mwili huo, likiwa tayari kuoondoka hospitalini hapo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Moshi kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment