TANGAZO


Wednesday, October 30, 2013

Muhubiri Deya kizimbani kwa ubakaji UK

 


Muhubiri Deya amekataa kurejea Kenya kwa hofu ya kutotendewa haki
 
Mhubiri mkenya aliyedai kuwa na uwezo wa kuwatunga mimba wanawake, kimiujiza, kupitia kwa maombi, ameshitakiwa kwa makosa ya ubakaji nchini Uingereza.
 
Polisi walisema kuwa Gilbert Deya, mwenye umri wa miaka 61, alishitakiwa wiki jana kwa kosa la ubakaji , kosa lengine la jaribio la kumbaka mwanamke pamoja na kumnyanyasa kimapenzi msichana mwenye umri wa miaka 14

 
Deya apokuwa Kenya alidai kuwa anaweza kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya kupata watoto kuweza kushika mimba baada ya kuwaombea.
Kwa mujibu wa jarida la The Guardian nchini Uingereza Mhubiri huyo alishitakiwa siku ya Ijumaa kwa makosa matatu na kuzuiliwa kwa muda katika mahakama moja mjini London akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake tarehe nane mwezi Novemba.

Deya alitoroka nchini Kenya alipokuwa anasakwa kwa madai wa kuwaiba watoto huku akiwahadaa wanawake kuwa angeweza kuwatunga mimba kwa kuwaombea.

Mkewe ambaye walikuwa wanashirikiana naye kwa kashfa hiyo alipatikana na na hatia ya wizi wa watoto na kwa sasa anatumikia kifungo chake nchini Kenya.

Hata hivyo mnamo mwaka 2011 waziri wa mambo ya ndani UingerezaTheresa May aliamuru mhubiri huyo kurejeshwa Kenya baada ya mahakama kukataa ombi lake la rufaa kukataliwa akitaka asirejee Kenya.
Serikali ya Kenya inadai kuwa aliwaiba watoto watano kati ya mwaka 1999 na mwaka 2004.
Wasiwasi ulizuka 2004 mara tu baada ya kipindi kimoja cha BBC radio 4 cha udadisi kwa Jina Face the Facts kupeperusha hewani shughuli zilizofanywa na Deya.

Wanawake ambao hawangeweza kutunga mimba ama waliokuwa wamepita umri wa kuzaa, waumini katika kanisa lake la Peckham Kusini mwa London waliahidiwa wataweza kupata watoto kimiujiza.
Lakini watoto hao walikuwa wanazaliwa katika zahanati bandia mjini Nairobi nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment