Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha
treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja
viungani mwa mji wa Nairobi.
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini
No comments:
Post a Comment