TANGAZO


Friday, October 4, 2013

Mpira wa Pete UTUMISHI yakung'uka Mahakama Nusu fainali ya SHIMIWI, yaingia Fainali, kucheza kesho

Taswira tofauti tofauti wakati timu ya mpira wa Pete ya Utumishi "Kombani Queens" ilipoingia fainali kwa kuikung'uta Mahakama mabao 51-28 katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea mjini Dodoma. Utumishi inatarajia kumenyana na Ikulu katika fainali za michezo hiyo kesho.


Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiwa tayari kwa mchezo kati yake na Mahakama katika mchezo wa Nusu Fainali ya michezo ya SHIMIWI.
Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiomba dua kabla ya kuanza kwa mpambano dhidi yake na Mahakama kwenye nusu fainali za mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma mapema leo.
Timu ya Mpira wa Pete ya Mahakama kabla ya kuanza mechi kati yake na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika mchezo wa nusu fainali za mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma leo.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi, Perice Makau (GS, wa pili kushoto), akijaribu kutoa pasi wakati wa mchezo wa nusu fainali za mashindano ya SHIMIWI kati ya timu hiyo na Mahakama, Mjini Dodoma mapema leo. Mbele yake ni wachezaji wa Mahakama Sharifa (WD), Ruth (GD) na Joyce Mfyuji (GK), wakijaribu kukaba mpira usitoke.
Mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi (wenye jezi za bluu) na Mahakama (wenye jezi za njano), ukiendela katika Viwanja vya Jamhuri, mjini Dodoma mapema leo.
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi (jezi za bluu), ikimenyana na na Mahakama (jezi za njano), katika nusu fainali za Mashindano ya SHIMIWI, mjini Dodoma mapema leo.
Wachezaji wa timu za mpira wa pete za Utumishi, na Mahakama wakipambana katika mchezo wa nusu fainali za mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma mapema leo. 
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi, Anna Msulwa (GA, wa kwanza kushoto), akijaribu kufunga bao wakati wa mpambano dhidi ya timu yake na ya Mahakama katika mchezo wa nusu fainali za mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma mapema leo. Mbele yake ni Ruth (GD) na Joyce Mfyuji (GK), wote wa Mahakama na Perice Makau (GS) wa Utumishi wakisubiri mpira. (Picha zote na Happiness Shayo-Utumishi)

No comments:

Post a Comment