TANGAZO


Thursday, October 3, 2013

Michuano ya SHIMIWI, timu ya Pete ya Utumishi yaingia fainali, yaikunguta Tamisemi

Taswira tofauti tofauti wakati timu ya mpira wa Pete ya Utumishi "Kombani Queens" ilipoingia fainali kwa kuikung'uta TAMISEMI katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma 'Kombani queens" imeshinda mpambnano huo kwa goli  38-28 na kuingia nusu fainali.
Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma "Kombani queens" ikifanya mazoezi mepesi kabla ya kuingia uwanjani kupambana na  TAMISEMI katika mashindano ya SHIMIWI Kiwanja cha Jamhuri mjini Dodoma.
Timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI ikifanya mazoezi kabla ya kupambana wenzao wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma "Kombani Queens" .
Timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI ikisalimiana na timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma "Kombani Queens" kuashiria mwanzo wa mpambano wao wa Mpira wa Pete kuwania kuingia nusu Fainali za SHIMIWI.
 Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma "Kombani queens"  Monica Aloyce (GK) (aliyeruka juu) akiondoa hatari kutoka kwa wachezaji wa timu ya TAMISEMI wakati wa mpambano dhidi ya timu hizo.
Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI Defroza Otilia (GA) akijaribu kutoa pasi wakati wa mpambano na Utumishi  mjini Dodoma, mbele yake akikabwa na mchezaji wa Utumishi Monica Aloyce (GK) .
Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma "Kombani queens" Elizabeth Fussi (C)akitoa pasi wakati wa mpambano dhidi ya TAMISEMI  katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma. Mbele yake ni mchezaji wa TAMISEMI Imelda Hango (C) akijaribu kumzuia .
Fatma Ahmed (GS) wa timu ya mpira wa Pete ya ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akichukua pasi kutoka kwa Anna Msulwa (GA) (aliye mbele yake) katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma. Utumishi iliifunga TAMISEMI mabao 38-28.

No comments:

Post a Comment