Timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria kabla ya kuanza kwa mechi kati yake na timu ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Timu ya mpira wa pete ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kabla ya kuanza kwa mechi kati yake na timu ya Wizara ya Katiba na Sheria katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikisalimiana na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria kabla ya mpambano katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Amina Ahmed (WD) akijaribu kutoa pasi wakati timu yake na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria zilipokutana katika mashindano ya SHIMIWI Dodoma.
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikimenyana na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria zilipokutana katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Perice Makau (GS) akijaribu kufunga wakati wa mpambano kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Perice Makau (GS) akijaribu kutoa pasi wakati wa mpambano kati ya timu ya Utumishi na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma.Utumishi ilishinda kwa mabao 40-8.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria Joyce Nkoliala (aliyelala chini) akipewa huduma ya kwanza baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mechi kati ya timu
ya mpira wa pete ya Utumishi na timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Katiba na Sheria mjini Dodoma.
Na
Happiness Shayo
Timu ya mpira wa pete ya
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imefanikiwa kuingia katika robo
fainali ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) yanayoendelea mjini Dodoma baada ya kuifunga timu ya Wizara ya Katiba
na Sheria mabao 40-8 jana katika viwanja vya Jamhuri.
Katika mchezo huo,Utumishi
iliendelea kufanya vizuri kwa kuwatumia wafungaji wake Perice Makau (GS) aliyefunga
mabao 16 na Anna Msulwa (GA) aliyefunga mabao 4 na kuipatia timu hiyo mabao 20
katika kipindi cha kwanza huku timu ya Wizara ya Katiba na Sheria ikifunga
mabao 5 kupitia wafungaji wake Hidaya Hoza (GA) aliyefunga mabao 4 na Rukia
Mlingi (GS) aliyefunga bao 1.
Kipindi cha pili cha
mchezo, mpira ulionekana kuelemea timu ya Wizara ya Katiba na Sheria baada ya
kufungwa mabao 20-3 na timu ya Utumishi.
Akiongea mara baada ya
mechi hiyo,kocha wa timu ya Utumishi Bw.Mathew Kambona alisema kuwa pamoja na
kufanya vizuri katika mechi hiyo lakini alitumia wachezaji wa kawaida na
kupumzisha wachezaji mahiri kwa ajili ya mechi ya robo fainali.
“Mchezo wa leo ni mzuri
lakini nimeamua kutumia wachezaji wa kawaida ili kujiandaa na mchezo wa robo
fainali kati yetu na TAMISEMI utakaochezwa jumatano ya wiki hii katika viwanja
vya Jamhuri”alisema Bw.Kambona.
Pia,Bw.Kambona alisema kuwa
timu ya Utumishi imejipanga vizuri ili kuhakikisha inaendelea na moto huohuo wa
kutoa vichapo kwa wapinzani wake hadi kufikia fainali za mashindano hayo.
Naye kocha wa timu ya
Katiba na Sheria Bw.Paulo Mathias alisema kuwa timu yake imekubali matokeo kwa
kuwa imezidiwa na timu ya Utumishi.
“Kufungwa ni kitu
kinachotokea ndani ya uwanja kwa hiyo sina budi kukubali matokeo kuwa timu
yangu imezidiwa uwezo na timu ya Utumishi”alisema Bw.Mathias.
Mashindano ya SHIMIWI yako
katika mtoano wa kuingia robo fainali ambapo washindi watafanikiwa kuingia nusu
fainali.Michezo inayochezwa ni mpira wa miguu,mpira wa pete,karata,kurusha
tufe,riadha na kucheza bao.
No comments:
Post a Comment