TANGAZO


Wednesday, October 16, 2013

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal Ashiriki Swala ya Idd El Hajj Msikiti wa Anwaar Msasani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. 
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria katika swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, leo asubuhi katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini wa dini ya Kiislam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini hao leo.

No comments:

Post a Comment