Takriban watu 17 wamekufa baada ya kutokea kimbunga kikali kilichopiga pwani ya mashariki ya Japan.
Kisiwa kilichopo kusini mwa Tokyo cha Izu Oshima kimeharibiwa vibaya na kimbunga hicho kiitwacho Wipha ambacho kimesababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko.
Watu wengi wamekufa wakati nyumba zao zilipowangukia huku wengine wakifukiwa na matope yaliyotokana na maporomoko ya ardhi. Hadi sasa watu 50 hawajulikani walipo.
Kazi ya kulinda mitambo ya nuklia ya Fukushima imekuwa ikiendelea lakini wafanyakazi wanasema wamekwepa uharibifu wa kimbunga hicho.
Katika mji wa Tokyo usafiri wa ndege umesitishwa, huku huduma za treni za mwendo kasi zimeahirishwa pamoja na shule kufungwa.
"Hiki ni kimbunga kikubwa kutokea katika kipindi cha miaka 10 baada ya kile kilichopiga Kanto katika eneo la Tokyo," Bwana Hiroyuki Uchinda, Mkuu wa Wakaka wa Hali ya Hewa nchini Japan, amewaambia waandishi wa Habari.
Kimbunga Wipha kwa sasa kimeanza kupungua nguvu yake wakati kikielekea eneo la Kaskazini mashariki.
Mlio wa mpasuko
Kimbunga kilisababisha upepo mkali na mvua kubwa kuwahi kutokea jumatano asubuhi.
Karibu nchi 5 sawa na sentimeta 12 za mvua ilinyesha katika muda saa moja katika kisiwa cha Izu Oshima karibu kilometa 120 kusini mwa Tokyo.
Kimbunga hicho kimesababisha maporomoko makubwa ya udongo kutoka maeneo ya milima na kusabisha mito kubadili mwelekeo.
Picha za televisheni zimeonyesha mabaki ya nyumba zilizojengwa kwa mbao zikiwa zimefunikwa na matope na kufunikwa na mabaki.
"Nilisikia mlio wa mpasuko na baadae miti kwenye milima ikadondoka chini" mwanamke mmoja katika kisiwa hicho alikiambia kituo cha televisheni cha NHK." na baadae matope na nyumba kuporomoka".
No comments:
Post a Comment