TANGAZO


Friday, October 4, 2013

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, atembelea Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati), akiwasili katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao, zilizopo jengo la TTCL, Mtaa wa Samora leo, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli za Serikali. 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari  leo, jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea taarifa  kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya Serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dk. Jabiri Bakari akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu mpango wa Serikali katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika shughuli za Serikali kupitia Tovuti Kuu mpya ya Serikali iliyoanzishwa  kwa lengo la kuboresha na kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma, kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika utoaji wa maamuzi yanayowahusu na kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi.
Baadhi ya viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao, iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue leo jijini Dar es Salaam.
Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya  www.egov.go.tz. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala hiyo, wakiwa kwenye mkutano wao na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala hiyo, wakiwa kwenye mkutano huo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Wakala hiyo, wakiwa kwenye mkutano huo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala hiyo, wakiwa kwenye mkutano wao huo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), wakati alipokwenda kutembelea Ofisi za wakala kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo, Dar es Salaam leo
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwabene (kulia) katika mkutano huo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Ofisi za wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo, Dar es Salaam leo
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA), kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment