Jamal Malinzi, Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Utendaji mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo, uliofanyika leo. Kulia ni Wallace Karia, Makamu wa Rais wa TFF.
Leodger Tenga, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, aliyemaliza muda wake akizungumza na kumpongeza Jamal Malinzi, Rais Mpya wa shirikisho 
Baadhi ya wafuasi wa Rais Mpya wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Bw. Jamal Malinzi wakishangilia na kupongezana mara baada ya kusikia matokeo ya uchaguzi huo yakionyesha Jamal Malinzi ameshinda. 
Baadhi ya wafuasi wa Rais Mpya wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Bw. Jamal Malinzi wakishangilia na kupongezana mara baada ya kusikia matokeo ya uchaguzi huo yakionyesha Jamal Malinzi ameshinda. 
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji, Mvela kutoka Iringa, hali ilibadilika kutokana na furaha, jambo lililopelekea kupata mshtuko wa moyo. Hapa akisaidiwa kutolewa nje ya ukumbi na wajumbe wenzake. 
Kutoka kulia ni Leodger Tenga Rais wa TFF aliyemaliza muda wake, mwakilishi wa FIFA Ashford Mamelodi na Henry Tandau, wakiwa katika chumba cha uchaguzi huo. 
Jamal Malinzi, Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania, TFF akimpongeza Makamu wake wa Rais, Wallace Karia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo. 
Leodger Tenga, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, aliyemaliza muda wake, akimpongeza Jamal Malinzi, Rais Mpya wa Shirikisho hilo, mara baada ya kushinda. Hapa siyo kwamba walikuwa wanalia bali walikuwa wakipongezana mara baada ya kazi kubwa ya kusaka ushindi huo.

No comments:
Post a Comment