Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mbaraka Batega, akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu udhibiti wa wahamiaji haramu kwenye maeneo yaliyopo nje ya Mikoa ya Operesheni Kimbunga, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo), Frank Mvungi. (Picha na Eliphace Marwa-Maelezo)
IDARA ya Uhamiaji ni moja ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyenye jukumu la
kuhakikisha kwamba Ulinzi na Usalama wa nchi unaimarishwa. Katika kusimamia
jukumu hilo kikamilifu, Idara ya Uhamiaji inatekeleza majukumu makuu ya Msingi
yafuatayo:
i.
Kuwezesha
na kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu nchini
ii.
Kutoa
huduma ya pasipoti au hati nyingine za safari kwa Watanzania wanaosafiri nje ya
nchi kwa shughuli mbalimbali.
iii.
Kutoa
huduma ya Vibali vya kuishi nchini pamoja na Pasi mbalimbali kwa wageni
wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.
iv.
Kufanya
misako, doria, kubaini na kuwakamata wahamiaji haramu nchini na kuwachukulia
hatua kwa mujibu wa Sheria zilizopo.
v.
Kuratibu
mchakato wa maombi ya wageni wanaoomba uraia wa Tanzania na kumshauri ipasavyo
Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa hatua ya uamuzi.
Majukumu
hayo ndiyo yanaipatia Idara ya uhamiaji wajibu wa kulinda na kuimarisha ulinzi
na usalama wa nchi, sambamba na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Uwezeshaji
na Udhibiti wa wahamiaji nchini
Tanzania
ni nchi inayofahamika sana duniani kwa ukarimu wa watu wake, ardhi yenye
rutuba, rasilimali mbalimbali na vivutio vingi vya aina yake kwa watalii.
Tanzania pia kutokana na historia yake ya amani na utulivu pamoja na imani ya
viongozi wake kuwa binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja, Tanzania imekuwa ni
kimbilio salama la wakimbizi wengi na wapigania uhuru kutoka mataifa mbalimbali
Barani Africa.
Tanzania
pia inazidi kuwa kivutio kwa wageni wengi kutokana na kuwa na fursa nyingi za
uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, madini, utalii n.k.
Hata hivyo, si wageni wote wanaoingia nchini wanafuata taratibu za kiuhamiaji
katika kipindi chote cha kuwepo hapa nchini. Hivyo, Tanzania kama zilivyo nchi
nyingine duniani inakabiliwa na changamoto ya kuwepo wahamiaji haramu.
Wahamiaji
haramu hao wanatokana na makundi makuu yafuatayo:
Wahamiaji
haramu walioingia nchini kabla ya uhuru pamoja na vizazi vyao.
Wengi walikuja kama manamba katika
mashamba ya wakoloni. Ingawa wengi wao wamefariki, lakini vizazi vyao bado
vipo. Wahamiaji haramu wa aina hii wengi wanapatikana katika mikoa mingi ya
mpakani, Tanga, Pwani na Morogoro. Hawa kwa mujibu wa historia yao ni miongoni
mwa wahamiaji “walowezi” hapa nchini. Kazi kubwa inayofanywa na Idara ya
Uhamiaji ni kuwatambua, kuwaandikisha na baadae kuishauri Serikali ipasavyo kuhusu
hatua za kuchukua.
Wahamiaji
haramu wanaotokana na kuwepo kwa makambi ya wakimbizi na wapigania uhuru
nchini.
Baada
ya nchi nyingi kupata uhuru, wapigania uhuru wengi waliondoka, lakini baadhi
vizazi vyao bado vipo hapa nchini na baadhi ya vizazi hivyo vinaishi isivyo
halali nchini. Aidha, wengine ni wale walioishi nchini kama wakimbizi na baadae
kutorejea nchini kwao pamoja na vizazi vyao. Wengi wa wahamiaji haramu hao wapo
katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mtwara Ruvuma, Morogoro.
Katika
kuwashughulikia Wahamiaji haramu wa aina hii, Idara imeweka utaratibu wa
kuwatambua kwa kuwaandikisha katika madaftari maalum ili kuwa na kumbu kumbu zao
sahihi na baadae kuishauri Serikali kuhusu hatua za kuchukua. Madaftari haya yameisaidia
Serikali kuwatambua Wahamiaji haramu katika Mikoa ya Kagera na Kigoma wakati wa
Operesheni “Kimbunga” inayoendelea hadi sasa.
Wahamiaji
wanaozidisha muda wa ruhusa ya kuwepo nchini.
Hawa
ni Wahamiaji wanaoingia nchini kihalali na kupewa muda maalum wa kuwepo nchini.
Baadhi yao muda huo unapokwisha hawaondoki, wanaendelea kuishi kwa kujificha na
kuukimbia mkono wa sheria. Wahamiaji haramu wa aina hii wanashughulikiwa kwa
kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani na kuwaondoa nchini.
Wahamiaji
haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
Hawa
ni wale ambao wanaingia nchini bila kufuata taratibu zozote za Uhamiaji. Wengi
wao wanatumia njia zisizohalali wakati wa kuingia nchini. Kundi hili linahusisha
Wahamiaji haramu wengi waliopo katika maeneo ya mipaka yetu na nchi jirani
pamoja na makundi ya Wahamiaji haramu wanaoingia nchini kutoka nchi za Pembe ya
Afrika (Somalia na Ethiopia).
Wahamiaji haramu wa aina hii
wanashughulikiwa kwa kuwasaka, kuwakamata na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa
sheria, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani na kuwaondoa nchini.
Udhibiti
wa Wahamiaji haramu katika maeneo yaliyopo nje ya Mikoa ya “Operesheni
Kimbunga”
Wakati
wa utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete la kuwataka majambazi, majangili na wamiliki wa silaha
kinyume cha sheria kujisalimsha na Wahamiaji haramu walipo katika Mikoa ya
Kagera, Kigoma na Geita kurudi nchini kwao kwa hiari, Idara ya Uhamiaji iliendelea
na shughuli za udhibiti wa wageni katika kipindi hicho kwenye Mikoa iliyopo nje
ya eneo la operesheni.
Katika shughuli hizo za udhibiti wa wageni, Jumla ya wahamiaji haramu 6,653 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa na kuchukuliwa hatua mbali kwa mujibu wa sheria. Mataifa ya Wahamiaji hao haramu na idadi yao kwenye mabano ni kama ifuatavyo:- Malawi (3,778), Burundi (696), Congo DRC (1,739), Kenya (147), Uganda (20), Pakistan (12), Somalia (31), Nigeria (23) na Msumbiji (20). Wengine ni India (16), China (09), Rwanda (40), Ethiopia (97), Komoro (10), Uturuki (03), Afrika Kusini (02), Bukina Faso (01), Liberia (02), Italia (01), Singapore (01), Libya (01), Bulgaria (01), Ghana (02) na Syria (01).
Katika shughuli hizo za udhibiti wa wageni, Jumla ya wahamiaji haramu 6,653 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa na kuchukuliwa hatua mbali kwa mujibu wa sheria. Mataifa ya Wahamiaji hao haramu na idadi yao kwenye mabano ni kama ifuatavyo:- Malawi (3,778), Burundi (696), Congo DRC (1,739), Kenya (147), Uganda (20), Pakistan (12), Somalia (31), Nigeria (23) na Msumbiji (20). Wengine ni India (16), China (09), Rwanda (40), Ethiopia (97), Komoro (10), Uturuki (03), Afrika Kusini (02), Bukina Faso (01), Liberia (02), Italia (01), Singapore (01), Libya (01), Bulgaria (01), Ghana (02) na Syria (01).
Wengi
wa Wahamiaji haramu hao wameondolewa nchini, wengine wamefikishwa mahakamani
wakati wengine uchunguzi dhidi yao bado unaendelea. Aidha, wapo walio halalisha
ukaazi wao nchini wakati wengine wameorodheshwa kwa ajili ya hatua zaidi.
Watanzania
Wahamiaji haramu katika nchi nyingine.
Wakati
Tanzania ikiendelea na udhibiti wa Wahamiaji haramu nchini, takwimu zilizopo
zonaonesha kwamba wapo watanzania ambao nao wanakiuka Sheria, Kanuni na
Taratibu za nchi mbalimbali wanazokwenda, ikiwemo kuingia na kuishi katika nchi
hizo wakiwa Wahamiaji haramu.
Katika
kipindi cha mwaka 2012, Jumla ya watanzania 1,263 walirejeshwa nchini kutoka
mataifa mbalimbali. Aidha, katika kipindi cha Januari-August, 2013 jumla ya
watanzania 715 wamerejeshwa nchini kwa makosa ya kukiuka taratibu za Uhamiaji
katika nchi walizokwenda, hususan Afrika Kusini.
Kwa
kuwa sasa tunaishi katika ulimwengu ambao watu wanasafiri kutoka nchi moja hadi
nyingine kuliko kipindi chochote kile katika historia ya binadamu, tunapenda
watanzania nao wasafiri nje ya nchi kwa ajili ya kunufaika na fursa mbalimbali
na tumekuwa tukiwawezesha kufanya hivyo.
Pamoja na nia hiyo njema ya Serikali, tunatoa wito kwa watanzania wenzetu kuheshimu Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo katika nchi wanazo kwenda, kama ambavyo tunapenda wageni nao waheshimu Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo hapa nchini. Kufanya hivyo sio tu kwamba kutatujengea uaminifu na uadhilifu katika jamii ya watu tunaoishi nao ugenini, bali pia kutajenga jina zuri na heshma kwa nchi yetu miongoni mwa mataifa mengine.
Pamoja na nia hiyo njema ya Serikali, tunatoa wito kwa watanzania wenzetu kuheshimu Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo katika nchi wanazo kwenda, kama ambavyo tunapenda wageni nao waheshimu Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo hapa nchini. Kufanya hivyo sio tu kwamba kutatujengea uaminifu na uadhilifu katika jamii ya watu tunaoishi nao ugenini, bali pia kutajenga jina zuri na heshma kwa nchi yetu miongoni mwa mataifa mengine.
Sote
tufahamu kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuvumilia Wahamiaji haramu,
bila kujali wanatoka taifa gani. Kila nchi inajitahidi kukabiliana na
changamoto hii ya Wahamiaji haramu. Tofauti ni mbinu zinazotumika kulingana na
mazingira na uwezo wa nchi husika. Ndio maana kwa mazingira ya jiografia ya
nchi yetu, mapambano dhidi ya Wahamiaji haramu ni endelevu bila kujali kama kuna
operesheni maalum au ni katika hali ya utendaji kazi wa kawaida.
Hitimisho:
Suala
la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni la kila mwananchi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama
peke yake haviwezi kutekeleza jukumu hili bila ushirikiano wa karibu na
wananchi. Wahamiaji haramu hawana kisiwa chao wenyewe, bali wanaishi ndani ya
jamii. Tunawashukuru wote
waliotupatia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yetu na tunaomba tuendelee
kushirikiana kuanzia mwananchi mmoja mmoja, viongozi wa ngazi mbalimbali,
wanahabari pamoja na vikundi mbalimbali vya kijamii.
No comments:
Post a Comment