TANGAZO


Wednesday, October 23, 2013

EAC yakumbwa na mgawanyiko

Bendera ya jumuiya ya Afrika mashariki
 
Serikali ya Tanzania imekosoa Muungano mpya wa hiari wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda ulioundwa hivi karibuni.
Serikali ya Tanzania imeuelezea kuwa unaenda kinyume na makubaliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda walikutana hivi Karibuni nchini Uganda ambapo walikubaliana kuanzisha miradi ya pamoja ya kimaendeleo katika nchi zao hatua ambayo haijapokelewa vema na Serikali ya Tanzania

Hii ni ishara ya hivi karibuni kuwepo kwa mgawanyiko katika nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hii si mara ya kwanza kuzuka tofauti katika Jumuiya hii ambayo imeundwa ikiwa ni mara ya pili baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977 ,wakati huo ikiwa na wanachama watatu tu yaani Tanzania,Kenya na Uganda.

Mgogoro huu wa sasa inaelezwa kuwa chanzo chake ni mkutano wa pande tatu uliofanyika mapema mwezi July mwaka huu nchini Uganda ambapo nchi za Kenya,Uganda na Rwanda zilikubaliana kuungana katika kufanya miradi ya kimaendeleo ya pamoja ndani ya nchi zao,muungano ambao unaonekana kuitenga Tanzania,huku Burundi hivi karibuni nayo ikijiunga na Muuungano huo na kuufanya kuwa wa nchi nne.

Tanzania inasisitiza kuwa kulipaswa kuwepo na mazungumzo na maafikiano miongoni mwa nchi wanachama kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imetaja kuwa nchi hizo zimekiuka makubaliano yaliyoko kwenye mkataba wa jumuiya hiyo.

Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye makao yake Makuu mjini Arusha haijasema lolote tangu kuanza Muungano huo wa nchi tatu na wala haijajibu malalamiko hayo ya Serikali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment