TANGAZO


Monday, September 30, 2013

Francis Miyeyusho amtwanga Sadiki Momba kwa point

Bondia Sadiki Momba (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi. (Picha zote kwa hisani ya www.superdboxingcoach.blogspot.com)


Bondia Sadiki Momba (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho, wakati wa mpambano wao, usiokuwa wa ubingwa, uliofanyika Jumapili, ukumbi wa  Friends Coner, Manzese, Dar es Salaam. Miyeyusho alishinda kwa pointi.
Refarii Sako Mtilya, akimnyoosha mkono juu bondia Fransic Miyeyusho, baada ya kumgalagaza bondia Sadiki Momba, wakati wa mpambano wao jana.
Bondia Mussa Sunga (kushoto), akipambana na Fahiri Awadhi wakati wa mpambano wao, uliofanyika jana Jumapili. Awadhi alishinda kwa point.
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto), akitoa maelezo ya DVD zake, zenye mapambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito, zenye msisimko zinazofanyika duniani kote. Kocha huyo wa mchezo wa masumbwi, alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis, Manny Paquaio, Mohamedi Ali, Floyd Mayweather na wengine.
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto), akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza mchezo wa ngumi.
Baadhi ya raia wa kigeni kutoka China waliokuja kumsapoti bondia Mussa Sunga, wakiwa katika picha ya pamoja na bondia huyo.
Mabondia wakijichagulia DVD za mapambano ya ngumi za Kimataifa zilizokuwa zikiuzwa na Kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila 'Super D' (wa pili kushoto), wakati wa mchezo huo jana.
Mashabiki wa mchezo wa masumbwi, wakipiga picha ya pamoja wakati wa mapambano ya mchezo huo jana.

No comments:

Post a Comment