TIMU ya Yanga leo imeonesha kwamba wanayodhamira ya kweli ya kumchukua mchezaji wa mahasimu wao wa Simba, Mrisho Ngassa kwa kumchezesha katika kikosi chao kilichojitupa Uwanja wa Taifa kupambana na timu ya 3 Pillars ya Nigeria, jijini Dar es Salaam leo.
Mchezaji huo, ambaye timu zote za Simba na Yanga, zimepeleka jina lake katika fomu za usajili wake Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili kuidhinishiwa alikabidhiwa jezi nambari 9 katika mchezo huo, mchezo ambao alionekana kuhaha sana lakini bila kuleta madhara kwa vijana hao wa Kinageria.
Wachezaji wa Yanga na 3 Pillars wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo baina yao, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)Makapteni wa timu hizo, wakipeana bendera za timu zao
Kikosi cha timu ya 3 Pillars cha Nigeria, kabla ya mchezo wao leo, Uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Yanga, kabla ya mchezo wao leo, Uwanja wa Taifa na 3 Pillars ya Nigeria.
Benchi la ufundi la Yanga.
Benchi la ufundi la 3 Pillars ya Nigeria.
Wacheaji Gabi Ekelojuoti wa 3 Pillar ya Nigeria na Juma Abdul wa Yanga, wakikamiana katika mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Said Bahanuzi wa Yanga, akijaribu kupenya katikati ya wachezaji wa 3 Pillars ya Nigeria, Agu Daniel (20 na Suluka Olanrewaju katika mchezo huo.
Suluka Olanrewaju wa 3 Pillar ya Nigeria na David Luhende wa Yanga wakiwania mpira wakati wa mchezo wao huo.
Said Bahanuzi wa Yanga, akimtoka Chukwuma Ejiogu wa 3 Pillars ya Nigeria.
Mrisho Ngassa akimtoka Chukwuma Ejiogu wa 3 Pillars ya Nigeria.
Mrisho Ngassa akipambana na wachezaji wa 3 Pillars ya Nigeria.
Haruna Niyozima wa Yanga ya Tanzania, akimkwatua Sholla Adeniran wa 3 Pillars katika mchezo huo.
Golikipa Tijan Adewale wa 3 Pillars akipangua mpira uliokuwa ukitaka kuingia golini wake katika mchezo huo.
Husein Javu wa Yanga (kulia), akiwania mpira wa juu na Paul Umue wa 3 Pillars ya Nigeria.
Mchezaji Mrisho Ngassa wa Yanga, akimtoka Paul Umue wa 3Pillars ya Nigeria, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Hussein Javu wa Yanga akipiga shuti lililozaa goli pekee la timu yake ya Yanga katika mchezo huo, ambapo timu hiyo, iliibuka na ushindi wa bao 1-0 hadi mwisho wa mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lao pekee walilolipata katika mchezo na 3Pillars ya Nigeria, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Hussein Javu wa Yanga (kulia), akikimbilia mpira na Sholla Adeniran wa 3 Pillars katika mchezo huo.
Ubao wa matokeo ukionesha matokeo ya mchezo huo.
Kijana shabiki wa Simba akiwakejeli mashabiki wa Yanga katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment