TANGAZO


Thursday, August 1, 2013

Rais Jakaya Kikwete amuaga mgeni wake, Waziri Mkuu wa Thailand, Bibi Yingluck Shinawatra akielekea nchini Uganda

Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa  ameambatana na  mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake  ya siku 3 nchini Tanzania. (Picha zote na Kassim Mbarouk, Aron Msigwa-Maelezo)
Waziri mkuu wa Thailand, Bi. Yingluck Shinawatra (kulia), akiangalia burudani kutoka kwa vikundi mbali mbali ya vijana, uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo, wakati alipokuwa akiagwa na  mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 ya kiserikali. 
Waziri mkuu wa Thailand, Bi. Yingluck Shinawatra (kulia), akiangalia burudani kutoka kwa vikundi mbali mbali vya vijana, uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo, wakati alipokuwa akiagwa na  mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 ya kiserikali. 


Rai Jakaya Kikwete pamoja na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Thailand, Bi. Yingluck Shinawatra (kulia), akiangalia burudani kutoka kwa vikundi mbali mbali vya vijana, uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo, wakati alipokuwa akiagwa na  mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa Thailand, Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo, jijini Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu wa Thailand, akisalimiana na kuagana na Mawaziri pamoja na watu mbalimbali, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo kabla ya kuondoka nchini kuelekea Uganda kwa ziara ya kikazi.

Waziri mkuu wa Thailand, Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
Waziri mkuu wa Thailand, Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, Said Sadiq, akipunga mkono kumuaga rasmi Waziri Mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jeneral Davies Mwamunyange (katikati), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman (wa pili kulia), walipokutana baada ya Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kuelekea nchini Uganda kwa ziara ya kikazi.

No comments:

Post a Comment