
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Asha Bilal, (wa pili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batrida Burian, na viongozi wengine wakati alipowasili Jijini Nairobi juzi Julai 30, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu, uliofanyika Jiji humo jana Julai, 31, 2013. Makamu anaondoka leo Jijini Nairobi kurejea nchini baada ya kumalizika kwa majadiliano hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake kutoka nchi za Maziwa Makuu, wakati walipokuwa katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu, alipoiwakilisha Tanzania katika majadiliano ya mkutano huo uliofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya jana Julai 31, 2013. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:
Post a Comment