Chanjo ya Malaria huenda hatimaye ikapatikana kutokana na utafiti wenye kuonyesha dalili nzuri za matumaini. Hii ni kwa mujibu wa watafiti
Watafiti waligundua kuwa chanjo hiyo ambayo inatengezwa nchini Marekani iliwalinda watu 12 kati ya kumi na watano kutokana na maambukizi. Hii ni baada watu hao kupewa viwango vya juu vya chanjo hiyo.
Njia ya kutoa chanjo hiyo sio ya kawaida kwa sababu inahusu kumdunga mtu sindano ya vimelea vya Malaria ambavyo havina nguvu sana ili kuweza kumkinga kutokana na maambukizi.
Utafiti huo umechapishwa katika jarida la utafiti wa kisayansi.
Mkuu wa utafiti huo, Daktari Robert Seder, kutoka katika kituo cha utafiti wa chanjo, Maryland, Marekani, alisema kuwa tumefurahishwa sana na matokeo lakini ni muhimu tuweze kuufanya utafiti huo kwa mara nyingine na kwa watu wengi.
Imejulikana kwa miaka mingi kuwa ikiwa mtu ataumwa na Mbu waliochomwa kwa miale ya radiation inaweza kulinda mtu dhidi ya kuambukizwa Malaria.
Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa inaweza kuchukua zaidi ya Mmbu elfu moja kumuuma mtu ili aweze kukingwa kabisa kutokana na Malaria na kuwa changamoto kubwa sana kwa utafiti wenyewe.
No comments:
Post a Comment