TANGAZO


Tuesday, August 6, 2013

Benki ya KCB yakabidhi vifaa tiba na kuzindua mpango wake wa kuchangia madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari jijini Dar es Salaam leo

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza na kunakili habari zilizokuwa zikitolewa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam leo kwa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam leo. Wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na wengine ni baadhi ya Madaktari wa hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kuwekea mgonjwa gesi, vilivyotolewa na benki ya KCB kwa hospitali hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), moja ya vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani, akiangalia moja ya vifaa tiba vya kumwekea mgonjwa gesi, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye (katikati), vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kwa hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa, akimkabidhi moja ya boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi, Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina.
 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.

Na Joyce Ngowi

BENKI ya KCB Tanzania imekabidhi vifaa vya matibabu (oxygen flow meters) venye thamani ya sh milioni 72 kwa uongozi wa Hospitali ya Mwananyamala.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa benki hiyo kutoa misaada kwa hospitali hiyo ambapo mwaka jana ilitoa vitanda 65 na vikabati vyake kwa ajili ya wadi ya kina mama na vitano kwa ajili ya kujifungulia.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mawasiliano na masoko wa KCB, Christina Manyenye alisema matunzo na matumizi mazuri ya vifaa vilivyotolewa vitakavyoifanya benki hiyo iongeze misaada kwa kituo kwa kituo chochote kilichokwisha saidiwa.

Alibainisha kuwa benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kutembelea vituo vyote ambavyo imetoa misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kujionea manufaa yatokanayo na misaada husika.

"Mwaka huu tumetenga kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwa ajili ya kusaidia jamii inayotuzunguka katika sekta za afya,elimu,wajasiriamali na sekta isiyo rasmi pia jamii zenye shida mbalimbali ikwemo maafa au vyakula,"alisema Manyenye.

Alisema kuwa mikoa itakayofaidika na mpango huo ni pamoja na Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Morogoro,Moshi na Zanzibar

No comments:

Post a Comment