TANGAZO


Thursday, July 18, 2013

Ubalozi wa Cananda na MISA TAN, watoa mafunzo kwa waandishi wa habari

Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kanda ya Tanzania (MISATAN), Mohammed Tibanyendera akimkaribisha Balozi wa Cananda Nchini Tanzania, Alexandre Leveque kufungua mafunzo ya  Waandishi wa Habari wa Tanzania kutoka vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini ,mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Haroub Hussein)
Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque akifungua mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari wa Tanzania kutoka vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kanda ya Tanzania (MISATAN) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini, mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam. Kulia Mwenyekiti wa MISATAN, Mohammed Tibanyendera. 
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque (kushoto) akimsikiliza  Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kanda ya Tanzania (MISATAN), Mohammed Tibanyendera muda mfupi baada ya kuyafungua mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali yalioandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na ubalozi wa Canada, mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Dar es Salaam.Katikati Mkurugenzi wa MISATAN, Andrew Marawiti.
 Waandishi wa habari mbali mbali wakimsikiliza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini , mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari mbali mbali wakimsikiliza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini, mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment