TANGAZO


Saturday, July 27, 2013

Thomas Mashali awafananisha Mada Maugo, Karama Nyilawila na midole yake


Bondia Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam. (Picha zote na Blogu ya Super D)
Bondia Thomas Mashal



Hatua hiyo ya Mashali inatokana na awali kupondwa na Maugo kuwa hana uwezo na ni heri akageukia biashara ya kuuza chapati, wakati Kalama akimkebehi kuwa ni kibonde wake.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili katika gym yake, Manzese, Dar es Salaam jana, Mashali alisema mabondia hao hawana uwezo wa kupambana naye kwa sasa na ni kama midoli kwake.
Mashali, ambaye atapanda ulingoni Oktoba 30 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kuzichapa na Maugo, yuko katika mazoezi makali kwa ajili ya pambano hilo kabla ya baadaye kupigana na Nyilawila.

"Unajua hawa ni kama midoli kwangu (huku akionesha midoli aliyoshika), na kwa kudhihirisha hilo nitaanza na maugo Oktoba 30 kumuonesha kuwa hatakiwi kuzungumza asichokijua," alisema Mashali.

Alisema anaamini uwezo wake wa sasa utakuwa wa juu zaidi ya Maugo na Nyilawila, ambapo alipata sare alipopigana na Nyilawila.

Katika pambano hilo la Mashali na Maugo la Oktoba 30, kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi, ambapo Ibrahim Class 'King Class Mawe' atapanda ulingoni kupambana na Halid Manje katika mchezo wa raundi sita.
Bondia Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam.
Bondia Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam.
Bondia Thomas Mashali akiwa amekumbatia midoli yake anayoifananisha na mabondia wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment