TANGAZO


Tuesday, July 2, 2013

Rais Jakaya Kikwete amuaga mgeni wake Rais Barack Obama, yeye na Balozi wa Marekani nchini watoa machozi wakati ndege ikiruka

Askari wa kikosi cha ulinzi wa Rais wa Marekani, wakiwa juu ya paa la Uwanja wa Ndege wa Zamani, wakiangalia usalama kabla na baada ya kuwasili kwa Rais wao, Barack Obama, uwanjani hapo, ambapo aliagwa rasmi na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma, waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu wa Mkoa Said Sadiki,  Wakuu wa Wilaya za Temeke, Sofia Mjema na wa Ilala, Raymond Mushi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima pamoja na viongozi wengine. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Hapa Askari hao, wakirekebisha vifaa vya mawasiliano wakiwa juu ya paa la Uwanja huo, wa Zamani.
Hapa Askari hao, wakifunga vizuri vifaa vyao hivyo vya mawasiliano uwanjani hapo.
Wananchi waliojitokeza kumuaga Rais Barack Obama wa Marekani wakipunga bendera za Tanzania na marekani, uwanjani hapo leo.
Moja ya ndege inayofuatana na ndege ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Airforce One, ikiwa uwanjani hapo ikisubiri kuondoka pamoja na Airforce One.
Hapa baadhi ya Makamanda na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi wakiwa uwanjani hapo kumsubiri Rais Obama awasili kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kulia), akiwa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, uwanjani hapo kusubiri kumuaga Rais Barack Obama wa Marekani.
Hapa anaonekana mmoja wa mbwa anayetumika katika ulinzi na walinzi hao wa Rais Barack Obama, akiwa katika kuangalia usalama uwanjani hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani baada ya kuwasili uwanjani hapo tayari kuagwa kwa safari yake ya kurejea nyumbani nchini Marekani baada ya kuamaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais Barack Obama wa Marekani, akisalimiana na kuagana na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Salva Rwemamu, katiakti yao akionekana Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema.
Rais Barack Obama wa Marekani, akisalimiana na kuagana baadhi ya viongozi, uwanjani hapo. Kushoto ni mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
 Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Mama Salima wakiwa na wageni wao, Rais Barack Obama na mkewe, Michelle wakiangalia ngoma za utamaduni pamoja na kuwaaga wasanii wa vikundi hivyo vya burudani, vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa kuwaaga uwanjani hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuongoza mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani kuelekea kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya kupigwa nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani ili kuagwa rasmi.
Rais Barack Obama, akiwapungia wananchi pamoja na viongozi waliofika uwanjani hapo kumuaga wakati akielekea kwenye ndege yake tayari kwa safai ya kurudi nyumbani nchini Marekani leo.
Rais Barack Obama, akizungumza na watoto wa Rais Jakaya Kikwete, waliofika uwanjani hapo kumuaga wakati akielekea kwenye ndege yake, tayari kwa safari ya kurejea nyumbani leo. 
Wake wa Marais Jakaya Kikwete, Mama Salma (kushoto) na Barack Obama, Michelle (kulia), wakiagana kwa kukumbatiana huku waume zao wakiwaangalia.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto) na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thanduyise Chiliza.
Airforce One ikiruka uwanjani hapo baada ya Rais Barack Obama kuagwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Airforce One ikianza kupaa baada ya kuruka uwanjani hapo.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakipungia ndege iliyomchukua Rais Barack Obama, wakati ikiruka uwanjani hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete akifuta machozi huku akiangaliwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakati ndege iliyombeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani ikiruka angani.
Hapa Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt na Rais Jakaya Kikwete, wote wakionekana kufinya macho yaliyokuwa yakilengwa lengwa na machozi baada ya ndege iliyokuwa imembeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani kuruka angani.
Hapa Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Mkuu wa Mkoa, Said Sadiki (kulia), wakifuatilia ndege hiyo, iliyokuwa tayari angani. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Hapa Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt akionekana bado akiendelea kufuta machozi huku  Rais Jakaya Kikwete (kulia), akimcheka pamoja na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anayeshikwa mkono na Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu mizengo Pinda.
Hapa Rais Jakaya Kikwete, anaonekana bado akibana macho yake.
Hapa Rais Jakaya Kikwete sasa akiwa ameweka vizuri mawani yake na kulia Mkuu wa Mkoa, Said Sadiki wakiangalia kwa vizuri ndege hiyo iliyokuwa ikipaa mawinguni.

Hapa Rais Jakaya Kikwete (kushoto), Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya mgeni wao, kuondoka salama nchini. 

No comments:

Post a Comment