TANGAZO


Wednesday, July 24, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Bilal afungua mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, awataka watunga sera kupitia upya sera za mipango miji Afrika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi 'Physical Sciences'  (COSTECH), Profesa Clavery Tungaraza, baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013. 

Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. 
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. 

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. 


Na Richard Mwangulube, Arusha
MAKAMU wa Rais, Dk. Mohamed Bilal amewataka watunga sera na watoa maamuzi barani Afrika kupitia upya sera za mipango miji ili miji iweze kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Akifungua mkutano wa Kimataifa unaojadili changamoto zitokanazo na ukuaji kasi wa miji, ongezeko la watu mijini na maendeleo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi jijini Arusha leo, Dk. Bilal alisema maafisa mipango miji wanatakiwa kubuni mipango bora itakayowasaidia wakazi wa mijini kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa miaka ya hivi karibuni yamekuwa ni changamoto kubwa.
 “Kuna haja kubadilisha mipango yetu ili miji iweze kuhimili ongezeko la watu pamoja na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Bilal.
Alisema kuwa asilimia 75 ya nishati inayotumika mijini na nje ya miji na pia asilimia 80 ya taka ngumu inazalishwa mijini na miji hutoa zaidi ya asilimia 60 ya hewa ya ukaa angani, hali ambayo huchangia kuongezeka kwa hali ya ujoto duniani.
Makamu wa Rais alisema katika miaka ya hivi karibuni bara la Afrika limekuwa likishuhudia ukame na mafuriko ya mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikichangia ongezeko la umaskini na kushuka kwa uchumi katika nchi nyingi.
 “Hali hii imekuwa ikiwaathiri sana watu maskini hususani wale wanaoishi kwenye makazi duni, hivyo ipo haja kwa watunga sera na watoa maamuzi kukaa chini na kubuni mikakati bora itakayosaidia kukabiliana na mabadiliko hayo,” alisisitiza, na kuongeza: “Miji mingi Afrika inaweza kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, kama nia na mipango mizuri itaandaliwa.”
 Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuwa na miongozo na sheria imara ambazo zitazuia watu kujenga kwenye mabondeni ambako kuna hatari ya kukumbwa na mafuriko na maporomoko.
Bilal ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nyuklia alisisitiza umuhimu wa watu kubadili tabia na kuacha mtindo wa kufanya mambo wa mazoea ili kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kuna haja pia kuwa na mipango ya pamoja ya kidunia itakayosaidia kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Akiwasilisha mada kwenye Mkutano huo, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Alphonse  Kyessi alisema asilimia 70 ya wakazi wa Dar es Salaam wanaishi kwenye maeneo yasiyopimwa  hali inayowafanya wakazi hao kukumbwa na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
“Hali hii ipo kwenye miji mingi barani Africa,” alisema Profesa Kyessi .
Alisema idadi ya watu waishio mijini imekuwa ikiongezeka karibu kila mwaka barani Africa. “Hivi sasa idadi hiyo imekuwa ikikua kwa asilimia 40 na tafiti zinaonyesha kuwa kufikia mwaka 2050 idadi hiyo itakuwa kwa asilimia 61.8.”
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema chuo chake kimeanzisha kituo maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi kuhusiana na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wataalam kwenye eneo hilo nyeti .
Mkutano huo wa siku tatu unaowakutanisha wataalam mbalimbali kwenye masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka Afrika na kwingineko duniani umeandaliwa Kituo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Chuo Kikuu cha Ardhi  na Shirika la Marekani la START Secretariat.

No comments:

Post a Comment