Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ivory Cost Kolo Toure kutoka Manchester City.
Toure mwenye miaka 32 amesajiliwa na Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba na Man City wanaomilikiwa na kampuni ya Etihad kumalizika.
Ameichezea City jumla ya michezo 102 baada ya kusajiliwa akitokea Arsenal mwaka 2009 kwa pound milioni 14, lakini alicheza mechi 18 pekee msimu uliopita na kujikuta akiachwa kwenye kikosi cha wachezaji wa Man City walioshiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kolo Toure anaenda Merseyside baada ya aliyekuwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo Jamie Carragher kutundika daruga huku hatma ya beki kitasa wa timu hiyo rais wa Slovakia Martin Skrtel ikiwa haijulikani.
Ameuambia mtandao wa klabu hiyo hatua hiyo ina maana kubwa kwake, na amejiunga na moja klabu bora nchini England.
"Nilipoondoka City ilikuwa ni muhimu kwangu kubaki England kwa kuwa ni ligi bora na kuja Liverpool ni hatua kubwa kwangu."
"Nimeichagua Liverpool kutokana na historia yake na hamasa ya wachezaji wanavyoitumikia timu yao." Alisema Toure.
Katika misimu saba aliyocheza Arsenal, Toure alishinda Kombe la FA mara mbili na alikuwa miongoni mwa kikosi cha Arsenal ambacho kiliandika historia ya kucheza ligi ya 2003-04 bila kufungwa hata mechi moja.
Mwaka 2011 alikosa kombe la FA walilochukua Man City kwa kufungiwa miezi sita kutokana kushindwa kufanya vipimo vya madawa ya kuongeza nguvu michezoni.
Toure ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Liverpool baada ya klabu hiyo kumsajili, Luis Alberto na Lago Aspas pamoja na mlinda mlango Simon Mignolet aliyesajiliwa akitokea Sunderland.
No comments:
Post a Comment