Ofisa wa Bunge, Christopher Kanonyele akifafanua jambo kwa wananchi kuhusu majukumu ya msingi ya Bunge kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye maonesho ya ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Dar es Salaam. (Picha zote na Owen Mwandumbya)Mwananchi akisikiliza kwa hisia maelezo kuhusu rungu la Bunge 'Siwa ya Bunge' na umuhimu wake katika vikao vya Bunge, kwenye maonesho ya sabasaba, Dar es Salaam leo.
Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja akifafanua jambo hatua kwa hatua namna miswada inavyowasilishwa bungeni hadi inapokuwa sheria kwa mwananchi aliyetembelea banda la Bunge, wakati wa Maonesho ya Sabasaba leo.
Wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo ya picha za waliowahi kuwa Maspika wa Bunge tangu kuanza kwake lilikiwa Baraza la kutunga sheria mwaka 1926 kutoka kwa Ofisa wa Bunge, Ismail Jimrodger. Muonekano wa Banda la Bunge kwa nje katika viwanja vya sabasaba.
No comments:
Post a Comment