Mkazi wa Mbagala, Halima Ibrahim (kushoto), akimweleza Ofisa wa Vodacom Tanzania, Pasco Magesa (katikati), jinsi anavyonufaika na Promosheni ya Cheka Nao. Vifurushi vya Cheka Nao, vinawawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu. Ili kujiunga, mteja anatakiwa kupiga *149*01#. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Vodacom Tanzania. Matina Nkurlu. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
Ofisa wa Vodacom Tanzania, Rehema Meleki (wa pili kulia), akimwelezea John Mhiza (kushoto), mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam jinsi ya kujiunga na ofa ya Cheka Nao, inayomwezesha mteja wa mtandao huo, kuongea bila mipaka na mitandao yote nchini. Kujiunga na Ofa hiyo, mteja anatakiwa kupiga *149*01#.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, jana ulifanya zoezi la kuwatembelea wakazi na wananchi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, sambamba na kuwafikishia huduma za usajili wa namba zao za simu pamoja na kuelimishwa juu ya huduma ya Cheka Nao na zinginezo kwa kwa ujumla.
Shughuli hiyo ilianza asubuhi kwa wahudumu wa mtandao huo kuzungumza pia na wateja wao, ambao walijumuika pamoja kupewa huduma hizo, huku ikienda sambamba na urudishwaji wa namba zilizopotea nyumba kwa nyumba na kufanyiwa pia usajili.
Akizungumza katika shughuli hiyo kutembelea wateja wao, Meneja Mauzo wa Vodacom, Kanda ya Mbagala, Idd Mawe, alisema kuwa lengo la kuwatembelea wateja wao ni kuwapa elimu inayohusu mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania, unaotumiwa na watu wengi huku ukiwa na huduma mbalimbali.
Alisema wateja wengi walijumuika pamoja na kupewa elimu inayohusu mtandao wao, huku wale wasiosajiliwa wakipewa fursa hiyo, jambo ambalo limepokelewa kwa furaha, baada ya kuwagogezea karibu huduma zao, huku wakikutana na changamoto nyingi, zikiwapo za wateja kutokuwa na uelewa juu ya usajili wa simu zao.
“Vodacom ni mtandao ulioenea Tanzania nzima, hivyo tumeamua kuja Mbagala na kusambambaza wahudumu wetu sehemu nyingi za Mbagala kwa ajili ya kupata huduma zinazohusu matumizi bora ya simu za mkononi, hususan za Vodacom.
“Naamini wananchi walitumia vyema nafasi hiyo, huku tukiamini kuwa utendaji kazi huu itaendelea, kwa ajili ya kufanya kazi kwa ushirikiano na wateja wetu kwa namna moja ama nyingine, hasa katika kipindi hiki ambacho ni lazima kila mteja awe amesajili namba yake,” alisema.
Kwa mujibu wa Mawe, wataendelea kufanya zoezi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kuwapatia elimu hiyo wateja wao, huku kitu pekee kinachohitajika ni kufika na kitambulisho halisi chenye picha kwa ajili ya kusajiliwa.
Huduma nyingine zinazotolewa na Vodacom ni pamoja na kuweka na kutuma pesa M-PESA, Cheka Nao, ambapo wateja anaweza kujishindia fedha taslimu mpaka kiasi cha Tsh Milioni 100 na kuboresha maisha yao kwa kupitia Mtandao huo ulionea nchi nzima.
No comments:
Post a Comment