Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.
Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua akaunti ya 'Chap Chap' ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.
Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika kumi
·
Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
- Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
- Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
- Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
- Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
- Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa Mauzo ya Nje wa NMB, Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB Chap Chap Account, mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing akimshukuru Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap.
Baadhi ya Maofisa wa NMB na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment