Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo, wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za Ligi Kuu ya Vodacom, zitakazotolewa Julai 3 jijini. Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi milioni 200, zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo. Kulia ni Meneja Mawasiliano na Habari wa Vodacom, Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mawasiliano na Habari wa Vodacom, Matina Nkurlu.
WADHAMINI wakuu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Kampuni ya Vodacom leo, imetangaza
kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3, jijini Dar es salaam.
Vodacom imekuwa ikisubiri
kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa – Taifa Stars za kusaka nafasi ya
kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha
tukio la kukabidhi zawadi hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema
katika msimu wa 2012/2013.
“Tulikuwa tukisbiri wakati
muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu kumalizika kwa ligi mwezi uliopita
mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa ari na nguvu timu yetu ya taifa katika
kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil,” alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Mwalim amesema maandalizi yote ya zoezi hilo
yamekamilika kwani hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu
baada ya ligi kumalizika zaidi ya timu ya taifa – taifa stars.
Mwalim amesema hafla ya
utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo
wachezaji wa vilabu ambao miongoni mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi
wa TFF na walimu wa timu ya taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu
moja tu la kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema
kuingiza maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.
Mwalim ametumia nafasi hiyo
kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la Soka – TFF na kamati ya ligi kwa
uvumulivu wao wakati wote ambapo Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka
wa kukabidhi zawadi.
“Tendo la kukabidhiwa
zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote anaeshinda, tumeona uvumilivu
mkubwa na wenzetu walituelewa wakati tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila
kuharibu concetratiuon ya taifa. Tumeonesha umoja wetu.”
Mbali ya mabingwa timu ya
Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia
zawadi za wachezaji na wadau wengine mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye
maeneo yao.
Vodacom itakabidhi zawadi za
fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika
nafsi ya pili hadi ya nne.
Wengine watakaonufaika na
zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora, mwalimu bora, timu iliyoonyesha
nidhamu na mfungaji bora.
Vodacom imekuwa ikiidhamini
ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya misimu mitano sasa huku
ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya ushindani kadri miaka inavyosonga
mbele.
No comments:
Post a Comment