TANGAZO


Monday, June 24, 2013

Tanzania yanyakua Tuzo tatu za ubunifu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika nchini Ghana


TANZANIA imenyakua Tuzo tatu za Ubunifu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika. Tuzo hizo zimetolewa wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika jijini Accra leo. 

Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana, jijini Accra ambapo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi, akimwakilisha Waziri wa Nchi-Utumishi, Celina Kombani (MB), ambaye pia ni Mwenyekiti wa mpito wa Mkutano wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika, alisema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa Umma Barani Afrika kujikita katika ubunifu ili kuleta tija kwa tasisi na wateja wanaowahudumia. 

Sherehe hizo, zimehudhuriwa na viongozi pamoja watumishi wa umma kutoka sekta mbalimbali barani Afrika. 

Awali, Mkuu wa Watumishi wa Umma nchini Ghana, Prosper Douglas Kweku Bani, alisema mchango wa watumishi wa Umma Barani Afrika unatambuliwa lakini mwisho wa siku atakayetia jitihada zaidi katika kazi yake lazima atunzwe ingawa "wote ni bora na lengo ni moja", alisema.

Katika tuzo hizo, Tanzania imenga'arishwa na Taasisi za Wakala wa Vipimo (WMA), Nida na NAO.

Hapa chini ni baadhi ya matukio yaliyojiri katika Ikulu ya Ghana, wakati wa hafla hiyo ya utoaji Tuzo za Ubunifu katika picha.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Watumishi nchini Ghana, aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, Propser Douglas Kweku Bani akitoa hotuba yake kabla ya utoaji Tuzo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi, akisoma hotuba yake katika Ikulu ya Ghana wakati wa utoaji Tuzo za Ubunifu kwa taasisi za Umma mbalimbali Barani Afrika.
Baadhi ya watumishi wa Umma kutoka Mataifa mbalimbali Barani Afrika, waliohudhuria hafla ya Utoaji Tuzo, wakiwa Ikulu ya Ghana-Accra, wakati wa utoaji wa tuzo hizo leo.



Wawakilishi wa NAO ya Tanzania,  wakipokea Tuzo toka kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Watumishi nchini Ghana, Propser Douglas Kweku Bani (kushoto), aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana jijini Accra leo.
Kikundi cha akinamama kutoka Kusini mwa Ghana kikionesha umahiri wake katika kucheza ngoma za utamaduni kwa kutumia vibuyu vikubwa viliyokatwa katikati. 
Kikundi cha akinamama kutoka Kusini mwa Ghana kikionesha umahiri wake katika kucheza ngoma za utamaduni kwa kutumia vibuyu vikubwa viliyokatwa katikati.
Bendi ya Jeshi la Polisi la Ghana, nayo haikua nyuma wakati wa utoaji Tuzo, hapa ilikuwa ikikoleza hafla hiyo.
Wawakilishi wa Wakala ya Vipimo nchini Tanzania (WMA), wakipokea Tuzo toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Watumishi nchini Ghana, Propser Douglas Kweku  (kushoto), aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana jijini Accra leo.
Raha ya Ushindi, wawakilishi wa NIDA ya Tanzania wakiserebuka na mgeni rasmi, Mkuu wa Watumishi nchini Ghana, Propser Douglas Kweku baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo leo.
Kikundi cha ngoma za Utamaduni nchini Ghana, kikitumbuiza wakati wa Utoaji Tuzo katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana-Accra.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi (katikati ya waliobeba Tuzo) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Tanzania baada ya kujinyakulia Tuzo tatu za Ubunifu, siku ya Utoaji Tuzo katika Ikulu ya Ghana-Accra. (Picha zote na Florence Lawrence-PO PSM)

No comments:

Post a Comment