Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Tamasha hilo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo Dar es Salaam leo, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ziff, Profesa Mhando, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Wananchi Programming, ambao ni wadhamini wa Tamasha la 16 la Ziff, Wangea Murange, akizungumza katika uzinduzi huo jijini leo. Kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando na katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Hannelie Bekker.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wananchi Programming, ambao ni wadhamini wa Tamasha la 16 la Ziff, Hannelie Bekker, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo jijini leo. Tamasha hilo, litafanyika visiwani Zanzibar, Juni 29 hadi Julai 7. Kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando na kushoto ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Wangea Murange.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Wananchi Programming, ambao ni wadhamini wa Tamasha la 16 la Ziff, Wangea Murange, akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando na katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya hiyo, Hannelie Bekker.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wananchi Programming, Hannelie Bekker, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 16 la ZIFF, Dar es Salaam leo. Tamasha hilo, litafanyika visiwani Zanzibar, Juni 29 hadi Julai 7. Katikati ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando na Meneja Mipango wa ZIFF, Ibrahim Mitawi.
Na Genofeva Matemu na Lorietha Laurence – MAELEZO
MAONESHO ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF), yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF, Profesa Martin Mhando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kuhusiana na tamasha hilo la 16 la Kimataifa litakalohusisha nchi za Jahazi.
Alisema dhamira kuu ya tamasha hilo ni kuhakikisha kuwa ZIFF inaleta mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini kwani imekuwa ikitoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wote na kuibua vipaji kwa kuzingatia kazi mbalimbali za sanaa na wasanii.
“Kupitia tamasha hili la 16 tunatarajia kutoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wa filamu mbalimbali na kuibua vipaji kwani mara nyingi tumekuwa tukifanikisha malengo ya wasanii mbalimbali na kuwawezesha kuwa wasanii mahiri katika tasnia ya filamu” amesema Prof. Mhando.
Naye Meneja Tamasha la ZIFF Bw. Daniel Nyalusi amesema kuwa tamasha limewahusisha watayarishaji wa filamu zaidi ya 35 mahiri kutoka nchi mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia ZIFF na kuwapa fursa hiyo maalumu kuongelea filamu zao na utengenezaji wa filamu kwa ujumla.
hapa nchini kuhudhuria kwa wingi na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wenzao toka nchi mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji vyao na kuweza kutoa filamu nzuri zitakazonyanyua soko la filamu hapa nyumbani.
“Miaka ya nyuma Tanzania hatukuwa na filamu nzuri katika soko la filamu hivyo kusababisha filamu za kinaijeria kuchukua nafasi kubwa na kuwafanya Watanzania wengi kufatilia filamu hizo ,lakini kwa kipindi hiki filamu zetu zimekuwa zikija juu kwa kasi kubwa sana hivyo kuua soko la filamu za kinaijeria kitu ambacho ni kizuri kwa taifa letu” amefafanua Bw. Nyalusi.
Alisema katika maandalizi ya tamasha hilo linalohusisha nchi za Jahazi ZIFF lilihusisha filamu 257 toka nchi mbalimbali ambapo filamu 80 zilifanikiwa kuchaguliwa, kuoneshwa ili kuweza kushindania tuzo za ZIFF za mwaka huu.
No comments:
Post a Comment