TANGAZO


Sunday, June 16, 2013

Taifa Stars, Ivory Coast zilivyopepetana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo

.Stars yakubali bao 4, mbele ya Ivory Coast

Wachezaji wa Ivory Coast wakiwa kwenye mstari kabla ya nyimbo za Taifa kupigwa, za Tanzania na nchin hiyo katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, nchini Brazil mwakani. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wakiwa kwenye mstari kabla ya kipute hicho kati yake na Ivory Coast kuanza Uwanja wa Taifa jijini leo.
Waamuzi pamoja na Maofisa wa mchezo huo, wakiwa kwenye mstari kabla ya kuanza kwa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa akiba na viongozi wa Ivory Coast wakiwa kwenye mstari wakiimba wimbo wa Taifa wa nchi hiyo.
Wachezaji wa akiba na viongozi wa Tanzania, wakiwa kwenye mstari wakiimba wimbo wa Taifa katika mchezo huo.
 Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mchezo kuanza leo.
Mashabiki wa Stars wakishangilia timu yao katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Taifa Stars na Ivory Coast wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu za Taifa Stars na Ivory Coast wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu za Taifa Stars na Ivory Coast wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Ivory Coast kikipiga picha ya kumbukumbu kabla ya mchezo huo.
 Kikosi cha Taifa Stars, kikipiga picha ya kumbukumbu kabla ya mchezo huo.
 Waamuzi wa mchezo huo, wakishauriana jambo kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akipambana na Bamba Souleman wa Ivory Coast.
 Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akijaribu kumzuiya na kumiliki mpira mbele ya Bamba Souleman wa Ivory Coast.
Bamba Souleman wa Ivory Coast akipiga mpira kichwa huku akizongwa na Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Amri Kiemba katika dakika ya pili ya mchezo huo.
 Mashabiki wa Stars, wakishangilia goli hilo.
Ubao wa matangazo ukionesha matokeo hayo katika dakika ya pili ya mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mbwana Samata wa Taifa Stars, akipambana na Zokora Didier wa Ivory Coast katika mchezo huo.
 Thomas Ulimwengu, akikokota mpira mbele ya wachezaji wa Ivory Coast.
 Thomas Ulimwengu, akikimbilia mpira na Bamba Souleman wa Ivory Coast.
  Thomas Ulimwengu, akiwa king'ang'anizi kuwania mpira huo na Bamba Souleman wa Ivory Coast.
 Mchuano wa Thomas Ulimwengu na Bamba Souleman wa Ivory Coast, ukiendelea hapa.
 Hatimaye Ulimwengu anafanikiwa kumtoka Bamba Souleman wa Ivory Coast katika mpambano huo.
Golkipa wa timu ya Taifa ya Ivory Coast, Barry Boubacar, akiuondoa mpira kwenye vichwa vya wachezaji, wakati mpira ulipoelekezwa golini kwake katika mchezo huo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Brazil, Uwanja wa Taifa dhidi ya Stars. 

Thomas Ulimwengu (kushoto), kazini tena na Bamba Souleman wa Ivory Coast katika mpambano huo.
Mara hii, Bamba Souleman wa Ivory Coast anafanikiwa kuuondoa mpira huo miguuni mwa Thomas Ulimwengu wa Stars.
 Mashabiki wa Stars wakifanya vimbwanga vyao kwenye mchezo huo.
 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
 Wananchi na wageni, waliokuwa wakiishabikia timu ya Taifa Stars, wakifuatilia mchezo huo.
 Haya ni matokeo ya kipindi cha kwanza kabla ya mchezo huo kuwa katika mapumziko.
 Thomas Ulimwengu na mpizani wake Bamba Souleman, wakikimbilia mpira katika kipindi hicho.
 Hapa mafahali hao, Thomas Ulimwengu na mpizani wake Bamba Souleman, wakiendelea kukamiana.
Kazi hapa inaendelea kuwa hiyo hiyo kwa Thomas Ulimwengu na mpizani wake Bamba Souleman kukamiana.
 Hatiamaye Souleman anaamua kufunga kazi kwa kukata kwanja lakini bila mafanikio.
Mashabiki wakishangaa vitendo vilivyokuwa vikitendeka vya kuoneshana ufundi katika mchezo huo kati ya wachezaji wa timu hizo mbili.
Hali ilibadilika kwa Stars na kukubali kupachikwa goli la tatu kama inavyoonekana katika ubao wa matangazo, uwanjani hapo.
Vijana wa Taifa Stars wakitoka kwa mapumziko baada ya kumalizika kipindi cha pili wakiwa nyuma kwa bao moja.
 Mbwana Samata, akichanja mbuga kuelekea golini huku akikimbizwa na mchezaji wa Ivory Coast.
Mbio hizo zilikatizwa na teklingi hii miguuni mwa Mbwana Samata, wakati akichanja mbuga kuelekea golini mwa Ivory Coast.
Dakika za mwisho hali inakuwa mbaya zaidi kwa Taifa Stars kwa kukubali kupachikwa goli la nne kama ubao huu wa matangazo ulivyokuwa ukionesha uwanjani hapo.
 Wachezaji wa Ivori Coast wakiwaaga na kuwashukuru Watanzania kwa ukarimu na uungwana wao.
Hapa akina Yaya Toure pamoja na wenzake wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo, walioshinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Taifa Stars na hivyo kufuzu kwa fainali hizo.
Yaya Toure akibanwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Jackson Odoyo wakati akitoka uwanjani.
 Wachezaji hao wakitoka uwanjani.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Ivory Cost.
Mashabiki waliojazana wakitaka kuwaona wachezaji wa Ivory Coast na kushikana nao mikono.
Mgeni rasmi katika mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo.

No comments:

Post a Comment