Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamadi, wakati wa ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar.
Ras wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kushoto akiwa pamoja na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada wakifungua kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein watatu kulia akionyeshwa mashine yenye kusambaza Umeme katika sehemu mbalimbali za Zanzibar na Meneja wa ZECO, Hassan Ali Mbarouk katika Ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiteta jambo na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban katika ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban, akitoa hotuba na kumkaribisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ili kuwahutubia wafanyakazi na wananchi katika ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo alipotoa hotuba wenye Ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada na kulia ni Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Wafanyakazi wa Zeco katika Ufunguzi wa kituo cha mradi wa uimarishaji miundombinu ya usambazaji wa Umeme kilichojengwa kwa msaada wa JICA hapo mtoni Mjini Zanzibar.
Na Faki Mjaka
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema licha ya Zanzibar kupata umeme wa uhakika kutoka Bara, Serikali yake inatarajia kuanzisha uzalishaji wa umeme mbadala ili kujitegemea katika huduma hiyo.
Amesema Serikali imefanya upembuzi yakinifu ambapo tayari wataalam wamethibitisha uwezo huo kwa Zanzibar kujitegemea katika huduma hiyo, ambapo muda si mrefu taratibu zitaanza kufanywa.
Dk. Shein ameyasema hayo leo, alipokuwa akizindua Mradi wa Uimarishaji Miundo Mbinu ya Usambazaji umeme huko Mtoni Zanzibar uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan JICA.
Amesema Utafiti uliofanywa umebainisha kuwa Zanzibar inaweza kutumia njia ya Upepo na Jua na kuweza kuzalisha Megawati 50 ambazo zitasaidia pale tatizo la umeme litakapotokea Tanzania Bara.
“Serikali imekuwa ikitafuta njia mbadala za kuzalisha umeme hapa hapa na utafiti umeonesha matokeo mazuri kuwa njia ya Upepo na Jua zinaweza kuzalisha hadi Megawati 50 ambazo zitatupa uhakika ili kule Bara hata kama kutatokea tatizo tuweze kuwa na umeme wetu ” Alisema Dkt. Shein.
Aidha ametaja njia nyingine mbadala ambazo Zanzibar inaweza kuzitumia kuzalisha umeme kuwa ni pamoja na njia ya Mawimbi ya bahari, Gesi na Takataka.
Dkt Shein ameelezea matumaini yake ya umeme wa uhakika unaopatikana kupitia msaada wa Japani kwamba utachochea sekta za maendeleo na ukuaji wa Uchumi.
Aidha amewataka viongozi wa Shirika la Umeme ZECO kutumia fursa hiyo ya upatikanaji wa umeme kudai madeni wanayowadai wateja wao wa Sekta binafsi, Taasisi za umma na Wananchi kwa ujumla.
“Tumuieni fursa hii kuwadai wote iwe ni Tasisi binafsi au Taasisi za Umma lakini mutumie njia za kistaarabu kudai madeni yenu ” Alieleza Dkt. Shein.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada amesema nchi yake itaendelea kuisaidia Zanzibar katika Sekta mbalimbali ili kudumisha urafiki wa muda mrefu baina ya Zanzibar na Japan.
Amesema ana matumaini kuwa Umeme wa uhakika ulipo Zanzibar utakuwa ni kichocheo kikubwa cha Maendeleo na fursa ya kukabiliana na umasikini nchini.
Awali akimkaribisha Rais Shein, Waziri wa Ardhi,Makazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban amewataka wananchi kuitunza na kuwa walinzi wa miundo mbinu ya umeme kwa kuepuka kujenga katika maeneo yaliyopita nyaya za umeme ili kuinusuru nchi kupata hasara.
Mradi wa Uimarishaji Miundo Mbinu ya Usambazaji umeme kwa kisiwa cha Unguja umefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo jumla ya Shl. Bilioni 57 zimetumika kugharamia ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment