Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Benki ya NMB, Diana Kimaro mara alipotembelea banda la benki hiyo, katika maonesho yanayoendelea kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
Mbunge wa viti maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zainab Vulu, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Huduma za Ziada wa benki ya NMB, Alluthe Nungu wakati walipotembelea banda la NMB katika maonesh hayo.
Baadhi ya Maofisa wa benki ya NMB, waliopo kwenye maonesho ya taasisi za kifedha, mjini Dodoma, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao, Viwanja vya Bunge leo, mjini Dodoma.
Ofisa Uhusiano wa Benki ya NMB, Doris Kilale (wa pili kushoto) akitoa maeleza kwa Mbunge wa viti maalum, Mathew Mlacha na Mbunge wa Busega, Titus Kamani juu ya huduma mbambali zinazotolewa na benki ya NMB.
No comments:
Post a Comment