Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba |
Na Baltazar
Mashaka, MWANZA
MWENYEKITI wa
Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema chama hicho
hakijawahi kuwa na sera ya ushoga kama ilivyoelezwa bungeni na Waziri Kivuli wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mbunge wa Nyamagana , Ezekia Wenje
(CHADEMA).
Alisema Chadema
imeishiwa siasa, inafanya siasa za kitoto na ni chama cha kihuni
kwa kutangaza uongo bungeni ilhali wao ndio wenye chama rafiki cha
Uingereza kinachokumbatia ushonga na ndoa za jinsia moja.
Lipumba alisema alitarajia Chadema kuzungumzia mambo ya msingi wakati huu ambao nchi inakabiliwa na mambo makubwa, badala ya kuibuka na sera za ushoga .
Alisema chama kinachopigania kuleta ukombozi wa wananchi wake kamwe hakiwezi kutumia lugha ya matusi katika jamii na ni wakati wa kuwa umoja kuliko wakati wowote ule katika kipindi hiki ambacho nchi iko kwenye matatizo makubwa.
Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo leo jijini Mwanza, katika mahojiano na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufunga semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali.
“Kashfa ya ushoga,Chadema wameishiwa siasa.Nchi inakabiliwa na mambo makubwa ya mpaka wa Malawi na waasi wa Rwanda,badala ya kutazama mambo ya msingi,Chadema wameibuka nakuzungumnzia ushoga, tena Wenje anazungumza kwa kukosea,”alisema Profesa Lipumba
“Hatuna sera ya ushoga ingawa kweli tuna uhusiano na vyama rafiki vya mrengo wa kati (Liberal International), Chadema wao mrengo wa kulia, wana urafiki na Conservative cha Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon.Wamebadili hilo na wanafanya siasa za kitoto. Msingi wa Liberali ni uhuru na haki ,”
Mwenyekiti huyo alihoji kuwa Je, Watanzania wafanye maandamano ya kupinga ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama sababu naye aliunga mkono ndoa za jinsia moja baada ya makamu wake Biden kushabikia vitendo vya ushoga.
Alisisitiza kuwa nchi ina matatizo mazito yanayotakiwa kutafutiwa ufumbuzi na chama kinachopinia kuleta ukombozii hakipaswi kutumia lugha ya matusi kwa jamii, hivyo Chadema ni chama cha wahuni na wameishiwa.
“Chadema hiki ni chama cha wahuni,wameishiwa sasa wanaleta masuala ya ushoga.Na ninawapa pole wananchi wa Nyamagana hamna mbunge hapa,”alisema Profesa Lipumba
CUF NA UDINI
Profesa Lipumba alitumia fursa hiyo kukanusha chama hicho kujihusisha na udini na yeye kumwunga mkono Rais Kikwete achaguliwe kwenye kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2010 akisema ni uongo na hakuwaji kusema wala kumwunga mkono.
“Huo ni uongo sikumwunga mkono JK.Kulikuwa na tetesi za udini na nilipokaribishwa mskitini kuzungumza nilihoji, mmepata nini na faida gani kwa kumpigania JK,na matunda gani mmepata kwa kampeni mliyofanya na hakuna aliyejenga hoja ya udhaifu wake,”
“JK aliahidi ajira, elimu bora, huduma bora za afya na maisha bora kwa kila mtanzania lakini hadi leo hakuna alichokitekeleza.Baadhi ya sera zangu CCM imezichota za kuondoa kodi ya kichwa ambayo ni ya manyanyaso, inavunja haki za binadamu.Elimu ya msingi na sekondari ni haki ya kila mtanzania,” alisma
Alisema kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana,akiwa meneja kampeni wa Rais Benjamin Mkapa, aliwahi kupinga sekta ya elimu kutlewaa chni ya asilimia 10 ya bajeti,ingawa sasa wamekubali.
VURUGU ZA MTWARA
Kuhusu chama hicho kutajwa vurugu za Mtwara, alisema serikali isitafute mchawi,sababu chanzo cha vurugu ni yenyewe baada ya kuahidimwaaka 2007/2008 kujenga kituo cha kufua umeme wa megawati 300 mkoani huo kwa kutumia gesi hadi sasa haijatekeleza kidai ya mtikisiko wa uchumi uliiathiri.
Kwamba nishati hiyo ingeingizwa kwenye gridi ya taifa na kusambazwa mikoa sita ya Kagera, Kigoma, Rukwa, Lindi, Ruvuma na Mtwara,ambapo serikali ilitumia bilioni 540 kutekeleza mradi wa umeme wa Mnazi bay katika kipindi cha mwaka 2010.
“Pale Mtwara zimegunduliwa futi za ujazo (Cubic feet) bilioni 80 za gesi,sasa serikali imejenga hisia kwa wananchi wa Mtwara na mikoa mingine kuwa hawataki rasilimali zao zitumike kwingine," alisema
Profesa Lipumba alisema kuwa JK anadanganya,hivyo akaitaka serikali hiyo ya CCM iwajibike kwa watu wa Mtwara iwaambie faida zitakazotokana na gesi badala ya kusema CUF inahusika katika kadhia hiyo.
|
No comments:
Post a Comment